Kijana wa miaka kumi na.. huko Marekani, amepoteza maisha baada ya 
kujipiga risasi bahati mbaya huku marafiki zake wakimuangalia kupitia 
Instagram Live.
Mama yake, Shaniqua Stephens amesema alisikia kishindo kikubwa kwenye
 chumba cha mwanae, Malachi Hemphill, 13. Yeye na mtoto wake wa kike 
walikimbia ghorofani na kumkuta mwanae akiwa amelala kwenye dimbwi la 
damu. Simu yake ilikuwa ikionesha Instagram Live.
Mtoto huyo alikuwa live Instagram akichezea bunduki kuwaonesha followers wake. Alikimbizwa hospitali ambako alipoteza maisha.
Polisi wanapeleleza kubaini ni kwa vipi Malachi alipata bunduki.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa













0 comments:
Post a Comment