Aliyelkuwa katibu mwenezi
wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema katika wilayaya Butiama Bw Richard
Choge Magori amekihama chama hicho kisha kuijunga na chama cha ACT
wazalendo kabla ya kuteuliwa kwa ajili ya kugombea ubunge katika jimbo
jipya la Butiama mkoani Mara.
Akizungumza baada ya
kukabidhiwa fomu na mkurugenzi wa wilaya ya Butiama kwa niaba ya tume ya taifa
ya uchaguzi ili kumwezesha kugombea ubunge katika jimbo hilo, kada huyo mpya wa
chama cha ACT- wazalendo, amesema kuwa ameamua kujiunga na chama hicho na
kugombea ubunge katika jimbo hilo baada ya kubaini wanachama
walipendekezwa kugombea
ubunge katika jimbo hilo mh Nimrod Mkono wa CCM na Bw Yusuf Kazi wa chadema
hawana uwezo wa kutatua matatizo ya wananchi wa jimbo hilo jipya.
Chanzo
ITV HABARI.
0 comments:
Post a Comment