William Bundalamahafu kwa (KIJUKUU CHA BIBI K )Mwandishi
wa habari na mtangaaji wa Radio Free Africa ameshinda kura za maoni katika nafasi ya
Udiwani katika kata ya Ulowa jimbo la Ushetu.
Akitangaza matokeo hayo Msimamizi wa uchaguzi huo
Sangoma amesema kuwa Bundala ameshinda nafasi hiyo kwa kupata kura 46 dhidi ya
Wagombea wenzake Charles Bahati aliyepata kura 14 na Marco Matheo ambaye
hakupata kura yoyote katika kinyang’anyiro hicho.
Kuelekea
uchaguzi mkuu Bundala alitangaza nia ya Kugombea Ubunge katika jimbo la Ushetu
na udiwani
katika kata ya Ulowa huku akisimamia kauli mbiu yake kuwa
“Tunahitaji mawazo na nguvu mpya za vijana kuleta mabadiriko ya maendeleo”.
Akiongea
kwa njia ya simu akiwa jimboni Bundala amesema kuwa huu ni mwanzo na kuongeza
kuwa kwa sasa anasubiri kura za maoni za ubunge ili kuchaguliwa kupeperusha
bendera ya Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema katika uchaguzi mkuu wa
mwaka 2015.
Sambamba
na hayo Bundala amesema kuwa Tanzania ilipofikia kwa sasa inahitaji viongozi
wazalendo wenye uchungu na rasilimali za wananchi na siyo kiongozi mwenye uchu
wa madaraka anayetaka uongozi kwa rushwa.
Kwa
upande wao wagombea waliokuwa katika kinyang’anyiro hicho cha udiwani wamesema kuwa
wameridhika na matokeo na kwamba lengo la CHADEMA ni moja kuleta mabadiriko
katika jimbo la Ushetu na kata ya ulowa kwa Ujumla.
Kwa
sasa Bundala anasubiri kura za maoni za Ubunge zinazotarajiwa kufanyika wiki
ijayo huku akiwa katika kinyang’anyiro hicho na watia nia wengine wawili ambao
ni Mabula Nkwabi na John Kitibu ambaye alipata kura 45 katika kura za maoni za
jimbo la Kahama Mjini katika uchaguzi ambao James Lembeli aliibuka mshindi.
0 comments:
Post a Comment