Hospitali
ya Taifa Muhimbili imegoma kuruhusu mwili wa marehemu Bi Hilda Lukas
miaka 30 aliyefariki dunia June 26 katika hospitali hiyo, akisumbuliwa
na ugonjwa wa utumbo kutoboka huku ikidai lazima fedha yote wanayomdai
marehemu ilipwe ambayo ni sawa na shilingi milioni moja na laki moja na
nusu kwa mujibu wa ndugu wa familia kama gharama za kumuhudumia mgonjwa
huyo.
Mama
wa marehemu Bi Anna Zuaro na Bibi wa marehemu wameiomba serikali na
wadau mbalimbali kuona namna wanavyoweza kuwasaidia kwani wao mpaka sasa
hawana fedha za kuuondoa mwili wa mpendwa wao, huku gharama za
kuuhifadhi mwili huo katika chumba cha kuhifadhi maiti zikizidi
kuongezeka.
Maafisaa
wa Muhimbili wanakiri marehemu Hilda Lukas alikuwa amelazwa katika wodi
ya kibasira chumba namba 9 ingawa haikuwa rahisi kuzungumza na maafisa
hao.
Uongozi
wa mtaa wa Chang’ombe umesema umefanya juhudi nyingi tu zikiwemo za
kuchangisha wananchi na wadau mablimbali lakini mpaka sasa bado
hawajaweza kukamilisha kiasi hicho cha fedha kinachohitajika Muhimbili
ambapo gharama za mochwari pekee mpka sasa ni shilingi 210,000.
0 comments:
Post a Comment