Naibu
Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson amesema wabunge wanawake
wamesikitishwa na kushindwa kwa mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya
Chama cha Democrat, Hillary Clinton.
Dk. Tulia alitoa kauli hiyo bungeni mjini Dodoma jana, baada ya kutambulisha wageni mbalimbali.
Alisema walitarajia mambo yangekuwa mazuri upande wao akiwa mama (wanawake), lakini haikuwezekana.
“Safari
hii haikuwezekana, asikate tamaa maana baada ya miaka minne mambo
yanaweza kuwa mazuri zaidi kuliko ilivyokuwa sasa. Nampa pole mama
Clinton kwa kuwa safari hii haikuwezakana,” alisema Dk Tulia huku akishangiliwa na wabunge wanawake na kuongeza:
“Nasikia kuna watu hapa wanasema tungempeleka mheshimiwa fulani… katika maeneo yale mama Clinton angeshinda,” alisema.
Kutokana
na kile kilichoonekana kupigwa butwaa na uchaguzi huo, kabla ya kuuliza
swali la nyongeza jana asubuhi, Mbunge wa Viti Maalumu, Suzan Lyimo
(Chadema), alisema ana masikitiko makubwa kwa sababu Hillary Clinton
ameshindwa uchaguzi.
“Kwa niaba ya wanawake wenzangu, nampa pole mama Clinton kwa kushindwa uchaguzi, tumeumia sana na tumerudi nyuma,” alisema.
Kauli
hiyo ilimfanya Dk. Tulia kumtaka aeleze amepata wapi taarifa wakati
bado wabunge wanawake wana faraja Hillary angeweza kushinda.
Hata
hivyo, akijibu swali la Suzan, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Khamis Kigwangala, alimpa pole
Hillary kwa kushindwa kwenye uchaguzi huo.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
Bonyeza Hapa CLICK HERE
<<<<DOWNLOAD APPLICTION KWENYE SIMU YAKO HAPA>>>
Bonyeza Hapa CLICK HERE
<<<<DOWNLOAD APPLICTION KWENYE SIMU YAKO HAPA>>>
0 comments:
Post a Comment