Ni jambo rahisi sana kushiriki tendo la ndoa na mpenzi wako, lakini cha kushangaza ni kwamba, ni wapenzi wachache sana wanaofanikiwa kufurahia kila hatua ya tendo. Na ndio maana wapenzi wengi hupoteza hamu ya tendo la ndoa mara baada ya muda mfupi tu wa mahusiano yao.
Radha ya tendo la ndoa ni muhimu sana katika ndoa yako, na kama radha ya tendo la ndoa itaanza kufifia usishangae kuona huduma zingine kuanza kufifia pia katika mahusiano yenu. Na kama unapenda kulifurahia tendo la ndoa na mpenzi wako, yapo mambo muhimu utatakiwa kuyazingatia kama ifutavyo:-
1. Usiwe mbinafsi.
Usiwe mbinafsi wakati wa tendo la ndoa; wapo watu ambao wakiridhika, huweza kuwageuzia kisogo wapenzi wao hata kama hawajafikishwa katika vilele vyao. Kama kila mpenzi atamjarimwenzie katika suala zima la tendo, furaha na upendo zaidi vitashamiri.2. Usitawanye mawazo yako.
Epuka kutawanya mawazo yako wakati wa tendo la ndoa, kwa kuhusisha mawazo yako ya pembeni yasiyohusiana na tendo la ndoa, kwakuwa hupunguza uwezo wa kuzama kikamilifu katika tendo.3. Andaa mazingira.
Kama unataka kulifurahia tendo la ndoa liandalie mazingira; mazingira safi ya kimahaba yatakuongezea urahisi wa kumfikisha kileleni. Kutokana na maelezo ya WHO juu ya Sexual Health “is the state of physical, imotional, mental and social well being in relation to sexuality” Mazingira ndio jambo la kwanza kuhusishwa hapo.4. Jifunze mitindo ya kuingiliana kimwili.
Kujifunza mitindo mbalimbali ya kuingiliana kimwili na mwenzi wako, haikusaidii kumfikisha kileleni pekee bali hukufanya uonekane mfalme au malkia hodari wa faragha. Utaweza kujifunza kuhusu mitindo na ubunifu mbalimbali wa kumwandaa na kumtawala mwenzi wako kila mara muwapo faragha;- hapa hapa kupitia www.hebronmalele.blogspot.com katika kategori yetu ya mahusiano……Usikose!!!5. Furahia kabla ya tendo la ndoa.
Kujifanyia nafasi ya kufurahia na mpenzi wako kabla ya tendo la ndoa, itakusaidia ufurahie zaidi tendo la ndoa, kwa mfano;- kushiriki chakula cha jioni (romantic dinner) pamoja, kufurahi pamoja na marafiki, kutazama sinema au vipindi vya tamthiria katika televisheni mkiwa pamoja na mpenzi wako, kabla ya kwenda kupeana mahaba, itakusaidia ulifurahie zaidi tendo la ndoa.6. Usiwe mzigo uwanjani.
Sababu kubwa inayopelekea wapenzi kutofurahia tendo la ndoa ni kukosa ujuzi wa faragha kwa kumlisha mapishi yaleyale ya kila siku! Inachosha mtu wangu….jifunze mbinu mpya uyanogeshe mahaba yenu. Kama umekosa mtu wa kukuongezea utundu,www.hebronmalele.blogspot.com tupo kwaajiri yako, usikose makala zetu za mahusiano kila siku.7. Mweleze mpenzi wako sehemu zinazokupa raha zaidi.
watu wengi huwaficha wapenzi wao kwa kutoweka bayana sehemu za miili yao, ambazo huwapa raha zaidi kama zikiguswa au kupapaswa. Hakuna baya lolote utakalo lifanya kwa kumweleza mpenzi wako sehemu zako nyeti unazopenda zipapaswe au ziguswe muwapo faragha. Msaidie mpenzi wako kupunguza ulefu wa safari ya kukufikisha kileleni.8. Punguza papala uwapo uwanjani.
Mara nyingi wapenzi hufanya haraka haraka kushiriki tendo la ndoa, lakini matokeo yake inapelekea mmoja wao kutofurahia hitimisho la tendo. Kama unataka kufurahia tendo la ndoa na mpenzi wako, msifanye papala kuanza na kumaliza tendo, acheni busu,denda, kupapasana na maneno ya kimahaba yachukue nafasi yake.Ni muhimu sana kuwa na maisha bora ya tendo la ndoa. Watafiti wamegundua kuwa, furaha ina mahusiano makubwa sana na tendo la ndoa, katika mahusiano. Hii ina maana kuwa ukiwa na maisha bora ya tendo la ndoa, itakusaidia kujenga mahusiano yenye furaha.
0 comments:
Post a Comment