Home »
Habari Moto
» #YALIYOJIRI>>>>Wilaya 43 ziko Hatarini Kukumbwa na Njaa.Fahamu zaidi hapa.
Serikali imesema kuwa nchi ina hifadhi kubwa ya chakula kutokana na
mavuno ya msimu uliopita ingawa kuna wilaya 43 zenye upungufu wa chakula
kutokana na mavuno yao kuwa chini hali iliyosababishwa na mabadiliko ya
tabia nchi.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha amesema hayo
jana wakati akizindua tovuti ya wakala wa hifadhi ya chakula nchini
(NFRA) mjini Dodoma.
Mhe. Ole Nasha amesema kuwa kwa sasa serikali ipo katika hatua za mwisho
za kuratibu uuzaji wa chakula nje ya nchi bila kuathiri hifadhi ya
chakula na kuwatoa hofu wananchi wenye wasiwasi wa kukumbwa na baa la
njaa.
Naibu waziri huyo ameongeza kuwa kwa tathmini waliyoifanya imebaini kuwa
nchi nyingi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika
zinakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula hivyo serikali itatengeneza
mifumo mizuri ya kupeleka chakula hicho nje ya nchi.
Baada ya kuzindua tovuti hiyo ya wakala wa chakula nchini, uhifadhi wa
nyaraka za serikali kwa njia ya makaratasi umepitwa na wakati lakini pia
akaongeza kuwa hata wizara nyingine zimeanzisha tovuti lakini ni kama
zimekufa kwa sababu haziweki taarifa za mara kwa mara.
Related Posts:
#YALIYOJIRI>>>>Makusanyo Kodi za Simu Yapanda Maradufu.Fahamu zaidi hapa.
Sheria
ya Fedha ya Mwaka 2016 iliyopitishwa kuhusu utozaji ushuru kwenye ada
ya kutuma na kupokea fedha kwenye miamala ya benki na simu, imeanza
kuzaa matunda kutokana na ongezeko la mapato lililoanza kushuhudiwa
kutok… Read More
Weka Picha za Utupu Mtandaoni Uende Miaka 20 jela – TCRA.Fahamu zaidi hapa.
Unataka kwenda jela? Ni rahisi, weka picha za ngono mtandaoni, na utakuwa mkazi wa huko kwa kipindi cha miaka 20.
Kwa mara nyingine tena, mamlaka ya mawasiliano Tanzania, TCRA
imewakumbusha watanzania kutozichezea sharubu… Read More
#YALIYOJIRI>>>>Lowassa, Mbowe Watakiwa Kuripoti Polisi Keshoi Septemba 1.Fahamu zaidi hapa.
Mwenyekiti
wa Chadema, Freeman Mbowe, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho, Edward
Lowassa na viongozi wengine waandamizi wameitwa na Jeshi la Polisi Kanda
Maalumu ya Dar es Salaam kwenda kuripoti kesho Septemba Mosi.
… Read More
#YALIYOJIRI>>>>Lowassa Atoa Waraka Kuhusu Kukamatwa Kwake.Fahamu zaidi hapa.
WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ametoa waraka akisema kitendo cha
askari wa Jeshi la Polisi kuwakamata wakati wakiwa kwenye kikao cha
ndani cha Chadema jana kimemuimarisha na kumpa nguvu zaidi ya kudai
demokr… Read More
#YALIYOJIRI>>>Jukwaa la wahariri lalaani Serikali kufungia redio.Fahamu zaidi hapa.
… Read More
0 comments:
Post a Comment