Aliyekuwa
Kocha wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa analidai Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF) Sh milioni 80 ikiwa ni fedha za malipo ya mshahara
wake ambazo hajalipwa kwa miezi kadhaa.
TFF
imeamua kuachana na Mkwasa hivi karibuni kwa makubaliano kufuatia
mkataba wake kutarajia kufikia tamati Machi, mwaka huu kisha kumteua
Salum Mayanga kushika nafasi yake hiyo.
Mayanga
aliyekuwa akiifundisha Mtibwa Sugar, ana jukumu la kuandaa kikosi
kitakachowania kufuzu Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (Chan)
Aprili mwaka huu.
Mshahara
wa Mkwasa kwa mwezi ulikuwa Sh milioni 28 ambao aliurithi kutoka kwa
Mart Nooij ambaye alisitishiwa mkataba kutokana na TFF kutoridhishwa na
utendaji wake.
Akizungumza, bosi
mmoja wa TFF alisema, Mkwasa anadai Sh milioni 80 ambazo anatarajiwa
kulipwa kwa mikupuo miwili ndani ya mwezi huu.
“Ni
kweli Mkwasa anaidai TFF Sh milioni 80 ambazo zinatokana na malipo ya
mshahara wake ambao ulikuwa ukilimbikizwa, hivyo TFF ipo katika hatua za
kumlipa fedha zake hizo kabla ya kocha mpya kuanza kazi.
“Fedha
hizo zinatarajiwa kulipwa kwa mikupuo miwili ndani ya mwezi huu ambapo
atalipwa katikati ya mwezi na mwishoni mwa mwezi,” alisema bosi huyo.
Alipotafutwa Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas, alisema kwa kifupi: “Hayo ni mambo binafsi ya mkataba, hayafai kuwekwa wazi.”
SOURCE: CHAMPIONI
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
0 comments:
Post a Comment