MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Nasib Abdul ‘Daimond Platnumz’,
amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa jitihada
zake kuhakikisha Dar es Salaam inakuwa salama.
“Kwanza kabisa Nimpongeze Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Makonda kwa
jitihada zake. Ukizingatia ni mwaka mmoja tu tokea awe mkuu wa mkoa
lakini utendaji wake umezaa matunda mengi na changamoto ni nyingi zinazo
mkabili lakini bado amekuwa imara.”, alisema Diamond.
Diamond ameyasema hayo leo katika mkutano kuhusu vita dhidi ya madawa
ya kulevya uliofanyika katika Bwalo la Polisi Oster Bay jijini Dar es
Salaam ambako Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, na viongozi wengine wa
serikali na taasisi mbalimbali walihudhuria.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment