Mwanamuziki
Diamond Platnumz amepata nafasi ya kuzungumza na Rais wa Tanzania, Dk.
John Magufuli kuhusu hali ya wasanii ilivyo nchini na kuomba serikali
kuunga mkono juhudi zao ili kulisaidia taifa kuongeza pato na wasanii
kupata faida kutokana na kazi wanazozifanya.
Diamond amezungumza
na Rais Magufuli kupitia kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa katika
kituo cha runinga cha Clouds Tv na kumwambia wamekuwa wakifanya jitihada
lakini zaidi wanahitaji msaada wa serikali ili wapate kipato ambacho
kinastahili kutokana na kazi wanayoifanya.
“Mkuu tunaomba
utusaidie sana maana tunaamini wewe ni Rais ambaye unatetea wanyonge na
kusaidia wanyonge na sisi vijana wako kwa unyonge wetu tunaomba
utusaidie kwasababu utakuwa umesaidia familia nyingi, sababu tuna
familia tuna watoto na watu wengi tunategemea mziki ili tujiajiri na
kuliingia pato taifa,
“Nafikiri tuweke system nzuri ya kulipa
kodi kama mimi ni mlipa kodi mzuri na wengine nimeweka mfumo wafate
hivyohivyo nafikiri itasaidia sana kuliingizia pato taifa na sisi pia
atleast kupata riziki na kujenga nchi yetu,” alisema Diamond.
Rais Magufuli alimjibu kwa kumpongeza kwa kazi nzuri ambayo wasanii wanaifanya ya kuitangaza Tanzania kimataifa, “Asante sana nimekusikia lakini pia nakupongeza na uzidi kuitangaza Tanzania katika muziki na hata wasanii wengine hata wale wanaoigiza nawapenda kama shilawadu na kadhalika.”
Lakini
awali akizungumza na mtangazaji wa kipindi hicho Babbie Kabae alisema
kuwa amepanga kukutana na wasanii ili kusikiliza changamoto
zinazowakabili, “Maombi yake nimeyasikia nimepanga siku moja kukutana na hao wasanii ili tuone jinsi gani tunawasadia.”
==>Tazama Video hapo chini
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment