Friday, 21 April 2017

Yusuph Mlela aomba pambano la ngumi na Nay wa Mitego.Fahamu zaidi hapa.

Msanii wa filamu nchini Yusuph Mlela aamemshutumu rapa Nay Wa Mitego kwa kile anachodai kuwa msanii huyo anapotosha jamii juu ya maandamano waliofanya baadhi ya wasanii wa filamu nchini.

Baada ya wasanii hao kuandamana wakipinga uingizwaji wa filamu za nje ambazo hazilipi kodi, kwa madai ziwaaribia soko lao la filamu za ndani, rapa Nay wa Mitego alisikika akisema kuwa baadhi ya wasanii wa filamu ambao waliandamana ni mataahira kwani kitendo cha wao kutaka filamu za nje zizuiliwe, hakina tija na mantiki yoyote.

“Walichokifanya baadhi ya Bongo Movie mataahira ni sawa na sisi wasanii tugome kuimba kisa nyimbo za wasanii wa nje zinapigwa sana Tanzania huyo ni utaahira,” alisema Nay wa Mitego kupitia video ambayo ameisambaza mtandaoni.

Kutokana na maneno ya kejeli ya Nay wa Mitego, muigizaji wa filamu Yusuph Mlela alishindwa kuvumilia na kuamua kumtolea povu rapa huyo.

“Nay True Boy wewe jamaa si ulikuwa chokoraa wewe, leo umeyapatia kidogo unasahau kwamba nyuma yako kuna kundi la vijana wanatamani kuwa waigizaji\wanamuziki wakubwa….Acha kupotosha jamii yetu Kwa sababu zako binafsi… sisi wasanii hatujakataza movie za nje. Tunataka wanaozisambaza wafuate taratibu za kisheria ili uwiano wa biashara uwepo ndiyo lengo la maandamano” aliandika Mlela Instagram.
Aliongeza, “Nay wa Mitego acha kutafuta sifa… nakushangaa kuwa na ufikirivu mdogo kama wewe siyo msanii…halafu huwezi kufananisha filamu na muziki….. Wewe si mtoto wa Manzese unajifanya unajua kupiga ngumi nataka Round 3 tu za boxing kwenye stage ili Tanzania ijue nani taahira nikutie adabu….. This is serous coz we mtoto mdogo tu kwangu ********** kuongea sana tabia za kike, wewe si hip hop na unajiamini njoo uwanjani chagua popote pale” Yusuph Mlela


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment