Wataalamu wa afya wamesema kwamba mlipuko huo unapatikana kwenye maeneo ambayo hayana usafi wa kutosha na vyoo vya kisasa hasa katika maeneo yenye msongamano wa makazi katika jiji hilo.
Maafisa wa afya tayari
wameshachukua hatua ili kuzuia mlipuko huo usienee zaidi tangu mlipuko mkubwa
wa kwanza ulioripotiwa kulikumba jiji hilo mwaka 2009.
Wodi
tengefu kwa wagonjwa wa ugonjwa huo imeshaandaliwa katika hospitali za wilaya
ya Kinondoni eneo ambalo limeathiriwa vibaya na ugonjwa huo.
Umma wa watanzania
wametakiwa kuwa waangalifu baada ya kifo cha mwanamke mmoja mwenye umri wa
miaka ishirini na saba,mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kuonesha dalili
zinazoshabihiana na magonjwa ya milipuko.
Dar
es salaam ni mmoja kati ya miji yenye idadi kubwa ya watu, mji huo pekee una
idadi ya watu zaidi ya milioni tano.Watu waishio katika makazi holela wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa ugonjwa wa kipindupindu kutokana na kutokuwa na vyoo bora na vya kisasa .
Chazo
BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment