Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akitoa hotuba fupi ya
kuwakaribisha nchini wajumbe wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na
Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha
Haramu (RECSA) kabla ya kufungua kikao cha wajumbe hao kinachofanyika katika
Hoteli ya Sea Cliff, Zanzibar. Lengo la kikao hicho ni kujadili
masuala mbalimbali ya jinsi ya Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa
Silaha Haramu katika nchi wanachama ambazo ni Burundi, Congo, Djibout,
Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda, Sudan, Sudan Kusini,
Seychelles, Afrika ya Kati, Somalia na Tanzania
Wajumbe wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za
Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti
Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) wakiwa katika chumba cha mkutano wakijadili
masuala mbalimbali ya jinsi ya Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa
Silaha Haramu katika nchi wanachama ambazo ni Burundi, Congo, Djibout,
Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda, Sudan, Sudan ya Kusini,
Seychelles, Afrika ya Kati, Somalia na Tanzania. Mkutano huo unafanyika katika
Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Sea Cliff, Zanzibar ambapo Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (hayupo pichani) ndio Mwenyekiti wa Baraza hilo,
hata hivyo katika Mkutano huo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira
Ame Silima (kulia meza kuu) anamuwakilisha katika kikao hicho. Mwakilishi
wa Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika
katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) na
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchini, Pereira Ame Silima (kulia) akiwa
na Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Uganda ambaye pia ni Makamu
Mwenyekiti wa Baraza hilo, Balozi James Baba (katikati) na Mjumbe wa Baraza
hilo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Usalama wa Ndani nchini Rwanda,
Balozi Munyabagisha Valeus, wakisoma taarifa za masuala mbalimbali ya jinsi ya
Kupambana ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu katika nchi
wanachama ambazo ni Burundi, Congo, Djibout, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda,
Sudan, Uganda, Sudan, Sudan Kusini, Seychelles, Afrika ya Kati, Somalia na
Tanzania. Baraza hilo limekutana katika Hoteli ya Sea Cliff, Zanzibar leo..
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Baraza la
Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia
na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) na Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani wa nchini, Pereira Ame Silima (kulia) akiwa na Waziri wa Mambo
ya Ndani nchini Uganda ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo, Balozi
James Baba (katikati) na Mjumbe wa Baraza hilo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa
Wizara ya Usalama wa Ndani nchini Rwanda, Balozi Munyabagisha Valeus, wakisoma
taarifa za masuala mbalimbali ya jinsi ya Kupambana ya Kuzuia na Kudhibiti
Uzagaaji wa Silaha Haramu katika nchi wanachama ambazo ni Burundi, Congo,
Djibout, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda, Sudan, Sudan Kusini,
Seychelles, Afrika ya Kati, Somalia na Tanzania. Baraza hilo limekutana katika
Hoteli ya Sea Cliff, Zanzibar leo.
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Baraza la
Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia
na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) na Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani wa Nchi nchini, Pereira Ame Silima (katikati waliokaa) akiwa katika picha
ya pamoja na Wajumbe wa Baraza hilo ambalo nchi zake wanachama ni Congo,
Djibout, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda, Sudan, Sudan Kusini,
Seychelles, Afrika ya Kati, Somalia na Tanzania. Wajumbe hao wamekutana katika
Hoteli ya Sea Cliff, Zanzibar leo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi. KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI WIZARA YA MAMBO YA NDANI
YA NCHI.
0 comments:
Post a Comment