Meneja masoko na mauzo wa Kampuni ya Mega
Trade Edmundi Rutaraka, akimkabidhi hundi ya Ts 1.5 Milioni Katibu wa
chama cha waandishi wa habari za michezo na burudani mkoa wa Arusha,Mussa Juma
kwa ajili ya tamasha la 10 waandishi wa habari mkoa wa Arusha, Manyara na
Dar es salam na wadau wa habari ambalo litafanyika Agoust 29 uwanja wa sheikh
Amri Abeid, hafla hiyo ilifanyika jana, Palace Hoteli Jijini. habari na
libeneke la kaskazini blog Tamasha la 10 la vyombo vya habari na wadau wa
habari mkoa wa Arusha, linatarajiwa kufanyika Agosti 29 katika uwanja wa Sheikh
Amri Abeid kwa kushirikisha timu nane ikiwepo timu ya TASWA kutoka jijini
Dar es Salaam. Akizungumza na waandishi wa habari, Palace Hotel , Katibu wa
chama cha waandishi wa habari za michezo mkoa wa Arusha(TASWA-Arusha), Mussa
Juma, alisema tayari maandalizi muhimu yamekamilika. Juma alisema Tamasha hilo
linaloandaliwa na TASWA na kampuni ya Arusha Media.mdhamini Mkuu ni Kampuni ya
Bia nchini( TBL) kwa miaka 10 sasa, litashirikisha michezo ya Soka, Mpira wa
pete, kuvuta kamba na kukimbiza kuku. "tunapenda kutangaza rasmi tamasha
la 10 ya TASWA Arusha litafanyika Agosti 29 na kauli mbiu yetu ni Uchaguzi Mkuu
bila vurugu inawezekana"alisema Alisema katika Tamasha hilo, ambalo
litashirikisha pia timu za wafanyakazi wa kampuni ya bia nchini(TBL) Taasisi na
Faidika na kampuni ya Pepsi litaandamana na ziara ya wanahabari kutembelea
Hifadhi ya Taifa ya Arusha.
PICHA ZAIDI
0 comments:
Post a Comment