Friday 14 August 2015

#YALIYOJIRI>>>Polisi yasitisha maandamano wakati wa kurejesha fomu NEC.




Jeshi la Polisi nchini limetangaza kusitisha maandamano ya aina yoyote wakati wote wa zoezi la kuchukua fomu za kuwania urais, kutafuta wadhamini mikoani na hata wakati wa kurejesha fomu kwenye tume ya taifa ya uchaguzi.

Uamuzi huo umetokana na kile polisi ilichosema ni sababu za kiusalama, hasa baada ya kuwepo kwa ukiukwaji mkubwa wa sheria za usalama barabarani kutokana na misafara mirefu iliyohusisha watu waliokuwa wakitembea kwa miguu, magari, pikipiki na baiskeli wakati wakiwasindikiza wagombea wa vyama vya Chadema na CCM.

Naibu inspekta Jenerali wa Polisi D/IGP Abdulrahman Kaniki akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam amesema manung'uniko na usumbufu uliojitokeza wakati za zoezi la wagombea urais wa CCM na Chadema kuchukua fomu tume ya taifa ya uchaguzi ni miongoni mwa sababu zilizosababisha kusitishwa maandamano hayo.

Akizungumzia kuhusiana na uamuzi huo huenda ukatafsiriwa kuwanyima haki wananchi ya kuamua kushiriki kwenye shughuli za kisiasa, Naibu inspekta Jenerali wa Polisi anafafanua zaidi.

Hivi karibu wagombea wa nafasi ya urais wa vyama vya CCM na Chadema wakiambatana na wafuasi wao walisababisha baadhi ya shughuli kwenye maeneo kadhaa jijini Dar es salaam kusimama kwa saa kadhaaa kutokana na maandamano yaliyokuwa yakielekea kwenye ofisi za tume ya taifa ya uchaguzi kwa ajili ya kuchukua fomu. 
Chanzo
             ChannelTEN

0 comments:

Post a Comment