Tuesday 11 August 2015

#YALIYOJIRI>>>Timu za Azam na Yanga zawazuia wachezaji kujiunga na timu ya Taifa Stars.




Charles Borniface Mkwasa kocha wa timu ya taifa ya Taifa Stars ameamua kufanya maamuzi ya ziada baada ya Timu za Azam na Timu ya Yanga kutowaruhusu wachezaji wake kujiunga na kambi ya Taifa Stars August 9 na badala yake kuendelea na maandalizi yao ya mchezo wa Ngao ya Hisani utakaopigwa August 22.

Wachezaji walioongezwa  kwenye kikosi cha Taifa Stars ni golikipa Saidi Mohamed, Vicent Andrew, kutoka Mtibwa Sugar, Mohamed Hussein (Tshabalala) na Ibrahim Ajib, kutoka Simba, Hamis Ally na Juma Mbwana kutoka KMKM, Tumba Swed kutoka Coast Union, Samwel Kamuntu kutoka JKT Ruvu na Ibrahim Hilka kutoka klabu ya Zima moto ya Visiwani Zanzibar sambamba na golikipa wa Tanzania Prisons Mohamed Yusuph ambae bado hajawasili

0 comments:

Post a Comment