WAKATI
Chama cha wananchi CUF ambacho ni chama kikuu cha Upinzani visiwani
Zanzibar kikiwa kimesusia uchaguzi wa marudio ambao unafanyika Marchi 20
ya mwaka huu,Baraza la Waislam (BAKWATA) limesema marudio ya
uchaguzi huo ndo njia ya kipee ya kurudisha amani visiwani humo..
Akizungumza na waandishi wa habari leo,Jijini Dar es Salaam, Sheikh Mkuu mkoani hapa,heikh alhadj Mussa Salum amesema Bakwata wanaunga mkono Tangazo la ZEC la kurudiwa kwa uchaguzi hu.
“Uchaguzi
huu wa marudio kwetu Bakwata tunaona ndio njia ya kipekee ya kukiweka
kisiwa cha Zanzibar kuwa sehemu ya Amani na utulivu,natumia nafasi hii
kuwaomba chama cha CUF kushiriki uchaguzi huu” Amesema Sheikh Salum.
Sheikh
Salum ameongeza kwa kusema kuwa hata kiongozi wa jumuiya ya Uamsho
Visiwani Zanzibar, Sheikh Farid Hadi Ahmad amemwandikia barua na
kumweleza kuwa kurudiwa kwa uchaguzi kutasaidia kurudisha Amani visiwani
humo.
Katika hatua nyingine, Baraza hilo
limeipongeza serikali ya awamu ya tano kwa jitihada mbalimbali
inazofanya za kuimarisha nidhamu, kubana matumizi na kukuza uchumi.
"Pia tunaipongeza serikali ya awamu ya tano, inayoongozwa na Mh. John Magufuli, kutokana na hatua mbali mbali inazozichukua zenye lengo la kuimarisha nidhamu hasa kwa watumishi wa umma, hatua mabazo zimeanza kuleta tija kubwa ka taifa letu kama wote hivi leo tunavyoweza kushuhudia jinsi pato la serikali likongezeka mwezi hadi mwezi”, alisema Sheikh alhadj Mussa Salum na kuongeza;
“Aidha tunaipongeza kwa dhamira yake ya kubana na kupunguza matumizi ya serikali, na badala yake kuelekeza fedha kwenye huduma za jamii na watanzania tumeshaanza kunufaika na huduma hizo kama vile suala la elimu bure."

0 comments:
Post a Comment