Msanii
mkongwe wa hip hop nchini, Afande Sele amefunguka na kusema serikali
ihalalishe matumizi ya bangi na si kukosoa juu ya hoja iliyotolewa na
mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma.
Ikiwa
imepita siku moja toka mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma (CCM),
kusema haoni sababu ya serikali kuzuia bangi kuwa zao la biashara kwa
maana haoni madhara yake huku akidai kwamba viroba vina madhara zaidi
kuliko bangi, Afande Sele amefunguka na kusema serikali ihalalishe
matumizi ya bangi na si kukosoa juu ya hoja hiyo ya Joseph Msukuma.
Afande
Sele amedai kuwa kuna nchi ambazo tayari wao wamehalalisha matumizi ya
bangi na kuthibitisha kuwa pombe ina madhara makubwa zaidi kuliko bangi.
"Legalize
it, Don't criticize it. Korea Kaskazini, Marekani, Mexico Uruguay na
mataifa mengine ya Ulaya yamethibitisha pombe ina madhara kuliko
Cannabis Sativa" Amesema Afande Sele.
0 comments:
Post a Comment