Serikali
 katika mwaka wa fedha 2016/2017 imepanga kuongeza ajira kwa vijana ili 
kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana wengi wa 
kitanzania kwa kuongeza ajira na kuwezesha wengine kujiajiri kupitia 
mifuko ya uwezeshaji toka Halmashauri za Wilaya nchini.
Akijibu
 swali la Mhe.Mgumba Tebweta Omary Mbunge wa Morogoro Kusini (CCM) lenye
 sehemu a na b lililouliza Serikali itaanza lini kuwawezesha vijana wa 
Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki  kifedha ili waweze kujiajiri na 
kuondokana na tatizo la ajira na umaskini ,Naibu Waziri Ofisi ya Rais 
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe  Suleiman Jafo 
amesema vijana katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Kusini Mashariki
 wamekuwa wakiwezeshwa kiuchumi kupitia fedha za Mfuko wa Maendeleo ya 
Vijana ambapo kila Halmashauri hupaswa kutenga asilimia 5 ya mapato yake
 ya ndani kila mwaka kwa ajili ya vijana.
Mhe 
 Suleiman Jafo ameongeza kuwa katika Bajeti ya mwaka 
2014/2015,Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro ilifanikiwa kutoa Shillingi 
Millioni 10.3 kwa vikundi vya vijana 19 kwa ajili ya kutekeleza shughuli
 mbalimbali za kiuchumi na katika Bajeti ya mwaka wa fedha 2015/2016 
vikundi vya vijana vilitengewa Shilllingi Millioni 87.5 ili kuviwezesha 
kiuchumi kwa kujiajiri.
“Katika
 kutatua changamoto zilizopo kwa vijana tunawawezesha  kifedha ili 
kujiajiri ili kumekuwa na tatizo la fedha kuchelewa kufika kwa walengwa 
ila Serikali kupitia Wizara yangu tunalifanyia kazi ili fedha zifike kwa
 wakati na tumetenga Shillingi Millioni 50 kwa kila kijiji kwa ajili ya 
kuwezesha vijana walioko katika vikundi mbalimbali mfano SACCOS ili 
waweze kujiajiri na kujikwamua kiuchumi kwa kujiondoa katika hali ya 
umaskini”
“Napenda
 kuwaomba wabunge tusaidiane sababu wao  wanahusika katika kamati za 
fedha za Halmashauri za Wilaya, waende wakasimamie hizo fedha kwa ajili 
ya kuwezesha vijana  zitoke na ziwasaidie walengwa” Alisema Mhe Jafo.
Aidha
 Mhe  Suleiman Jafo amesema kuwa Serikali imetenga Shillingi Billioni 
233 kwa ajiri ya kuajiri vijana wapya takribani 71,408 kati ya hao 
watumishi wapya wa Afya wanatarajiwa kuwa takribani 10,871 na Waalimu 
40,000 kwa nchi nzima ili kupunguza tatizo la ajira kwa vijana 
wanaomaliza vyuo mbalimbali nchini.
Serikali
 kupitia Halmashauri za Wilaya imejipanga katika kuwawezesha vijana 
katika maeneo yao kujikwamua kiuchumi kwa kujiajiri na kwa mwaka wa 
fedha 2016/2017 Serikali itaboresha zaidi mifuko ya kuwezesha vijana 
katika Halmashauri za Wilaya kwa kununua vifaa zaidi vya kujifunza stadi
 mbalimbali za kazi zitakazowezesha vijana wengi zaidi kuwa na ujuzi 
utakaowasaidia kujipatia kipato na kujikwamua kiuchumi.
 









 




 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment