Saturday 3 September 2016

#MICHEZO>>>>KIKOSI CHA SIMBA BILA MASTAA 6 KIMEPATA USHINDI DHIDI YA POLISI DODOMA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Simba SC imeifunga Poilisi Dodoma ya mkoani Dodoma magoli 2-0 kwenye mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu uliochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

Magoli ya Simba yamefungwa na Abdi Banda ambaye aliunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Mwinyi Kazimoto dakika ya 45+2 kipindi cha kwanza.
 Said Ndemla (kulia) akishangilia goli lake na Haji Ugando (kushoto) wakati wa mechi dhidi ya Polisi Dodoma kwenye uwanja wa Jamhuri, Dodoma
 Fredrick Blagnon (katikati) hakufanikiwa kufunga goli kwenye mchezo dhidi ya Polisi Dodoma licha ya kupata nafasi nyingi za kufunga lakini alishindwa kuzitumia

Said Ndemla alifunga goli la pili la Simba dakika ya 60 kwa shuti kali la umbali wa zaidi ya mita 22 ambalo lilimshinda golikipa wa Polisi Morogoro.

Mchezo huo ulikuwa ni wa kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano kuhamia mjini Dodoma ambako ni makao makuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Mwinyi Kazimoto (kushoto) alionesha kiwango cha juu kwenye mchezo huo kwa kutengeneza nafasi za kufunga ambazo hazikutumiwa vyema na Blagnanon na Lyanga.
 Blagnon (katikati) hakumaliza dakika 90 kufuatia kuoneshwa kadi nyekundu dakika za majeruhi baada ya kumchezea vibaya mchezaji wa Polisi Dodoma

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Tulia Akson alikua mgeni wa heshima kwenye mechi hiyo ambapo aliambatana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo Mh. Nape Nnauye pamoja na viongozi wengine wa serikali ya mkoa wa Dodoma.
 Simba ilitumia wachezaji wake wengi ambao hawapati nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo kutokana na wachezaji wengi wa timu hiyo kuitwa kuzitumikia timu zao za taifa. Ibrahim Ajib, Jonas Mkude, Mohamed Hussein, Shiza Kichuya, Muzamiru Yassin wote wapo Nigeria kwenye kikosi cha Stars wakati Laudit Mavugo yeye akiwa kwenye timu yake ya taifa ya Burundi.

0 comments:

Post a Comment