Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewataka
Makamishna Wasaidizi Waandimizi na Mananibu Kamishna wa Jeshi la Polisi
kufanya kazi kwa bidii zote bila ya kumuogopa mtu yeyote katika
kuhakikisha maslahi ya nchi yanawekwa mbele.
Rais
Magufuli ameyasema hayo leo Ikulu, Jijini Dar es Salaam alipokuwa
akiwaapisha wa umma waliopandishwa vyeo hivi karibuni na Rais mwenyewe
kutoka Makamishna Wasaidizi kuwa Makamisha Wasaidizi Waandamizi na
waliokuwa Makamishna Wasaidizi Waandimizi kuwa Manaibu Kamishna
Wasaidizi.
Amewataka watumishi hao wa umma kufanya kazi kwa moyo mmoja na kutenda haki kwa watu bila kujali cheo wala umaarufu wa watu.
Akitolea
mfano wa Askari wa Usalama barabarani Rais Magufuli amesema wamekuwa
wakishindwa kukamata baadhi ya magari yanayomilikiwa na baadhi ya
polisi kama Happy Nation na Buffalo pale yanapofanya makosa na pindi
wanapochukua hatua dhidi ya magari ya aina hiyo basi wanatishiwa
kushushwa cheo au kuhamishwa kutoka pale walipo.
"Nataka
mkafanye kazi kwa haki bila kuogopa mtu hata kama ni gari la IGP,
Waziri au hata Rais sheria lazima ichukue mkondo wake na mhusika wa gari
hilo atakwenda kujieleza polisi mwenyewe." amesema Rais Magufuli
Rais
Magufuli amewataka makamishna hao waliopandishwa vyeo kuhakikisha sekta
zote zinazotakiwa kulipa kodi kama bandari na utalii zinafanya hivyo
kama sheria inavyosema huku akiwashangaa wale wanaosema kuwa meli
zimepungua bandarini na watalii kupungua nchini.
“Meli
zilizopungua bandarini ni zile ambazo zimekuwa hazilipi kodi kwakuwa
sasa mianya yote ya kukwepa kodi imezibwa. Ni afadhali zile meli chache
zitakazolipa kodi kuliko nyingi ambazo hazilipi kodi na vivyo hivyo
katika sekta ya utalii ni bora watalii wasije kama hawataki kulipa VAT
iliyotengwa na Serikali,” amesema Rais Magufuli.
Aidha,
amewataka makamishna hao kwenda kupambana na Tatizo la watumishi hewa
katika maeneo yao ya kazi ili kuhakikisha tatizo hilo ambalo
limeigharimu serikali mabilioni ya pesa halijirudii tena na kama bado
lipo linatokomezwa kabisa.
Akiongelea
suala la Polisi Jamii, Rais Magufuli amewataka makamishna hao kufanya
kazi bila kujali utaratibu huo wa polisi jamii na kuongeza kuwa amekuwa
akiupinga utaratibu huo tangu akiwa Waziri wa Uvuvi na kusisitiza kuwa
dunia ya sasa ni tofauti na ile tuliyoizoea.
“Ilikuwa
unaweza kumkuta mvuvi katikati ya ziwa akiwa anafanya vitu kinyume na
sheria alafu unataka kuleta mambo ya polisi jamii kwa kuanzisha
majadiliano na mhalifu, hili halikubaliki na nililipinga kwani ni lazima
ifike mahali polisi aheshimiwe na tofauti iwepo kati ya polisi na raia
wa kawaida,” amesisitiza Rais Magufuli.
Jumla
ya Makamishna Wasaidizi Waandimizi na Mananibu Kamishna 60 wa Jeshi la
Polisi wamepandishwa cheo na Rais Magufuli hivi karibuni na leo wamekula
kiapo cha uadilifu isipokuwa Manaibu Makamishna wawili ambao wapo nje
ya nchi kwa mafunzo maalum.
0 comments:
Post a Comment