Home »
Habari Moto
» #YALIYOJIRI>>>>Msanii Diamond Atoa Msaada Wa Madawati 600 Kwa Mkuu Wa Mkoa Wa Dar Es Salaam Mhe. Makonda.Fahamu zaidi hapa.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akimpongeza Mkurugenzi wa
WCB, msanii Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' mara baada ya kumtembelea
ofisini kwake na kutoa mchango wake wa madawati yapatayo 600 kwa ajili
ya kuchangia maendelea ya mkoa.
Akiongea
katika makabidhiano hayo msanii huyo alisema ni jambo jema kwao kuweza
kujitolea mchango huo ili kuweza kumuunga mkono Mhe. Makonda katika
kukabilana na changamoto za elimu.
Mkurugenzi
wa WCB, msanii Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' akiongea mara baada ya
kukabidhi msaada wa madawati yapatayo 600 kwa mkuu wa mkoa wa Dar es
Salaam Mhe. Paul Makonda ili kuweza kupunguza tatizo la wanafunzi kukaa
chini. Makabidhiano hayo yalifanyika leo Juni 6, 2016 ofisini kwa mkuu
wa mkoa jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akitoa shukrani zake za
pekee kwa Mkurugenzi wa WCB, msanii Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' kwa
kuweza kutoa madawati 600 ikiwa ni mchango wake katika elimu ya kuweza
kufanya wanafunzi kukaa sehemu salama.
Mhe. Makonda alisema kuwa wakati
umefika kwa wasanii wakaweza kujitoa katika jamii ambayo imekuwa ikiwapa
wao sapoti na msanii Diamond amekuwa wa kwanza kuonyesha moyo wa pekee
kwa kurudisha fadhila.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akiwa katika picha ya
pamoja na uongozi wa WCB mara baada ya kumtembelea ofisini kwake.
Related Posts:
#YALIYOJIRI>>>>Kesi Ya Kamanda Godfrey Nzowa Dhidi Ya Kamanda Suleiman Kova Kuunguruma Leo.Fahamu zaidi hapa.
Kesi ya maofisa wawili waandamizi wa polisi kutaka kuuziwa nyumba ya
Serikali inaanza kunguruma leo katika kikao cha Mahakama ya Rufaa mjini
Arusha. Wanaopambana katika kesi hiyo ni Mkuu wa Kikosi cha
Kupambana na Dawa … Read More
#YALIYOJIRI>>>Shahidi :Nilimsikia Kubenea akimwambia DC Paul Makonda ni kibaka,mjinga, mpumbavu na cheo chenyewe kapewa.Fahamu zaidi hapa.
Mratibu
Msaidizi wa Jeshi la Polisi, ASP Denis Mujumba, 39 ameieleza Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa akiwa Mkuu wa Upelelezi Magomeni alimsikia
Mbunge wa Jimbo la Ubungo Saed Kubenea akimwambia Mkuu wa Wilaya ya
K… Read More
#YALIYOJIRI>>>Wanafunzi 21 Wafukuzwa Shule Kwa Muda Usiojulikana,Kosa Lao Ni Kuvaa "YeboYebo", Mwalimu Wa Zamu Alizichukua na Kuzichoma Moto.Fahamu zaidi hapa.
Wanafunzi
wapatao 21 wanaosoma Shule ya Msingi Kilambo cha Mkolechi, Kata ya Kala
mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilayani Nkasi, wamefukuzwa shule kwa muda
usiojulikana kwa kuvaa viatu maarufu yeboyebo.
Imeelezwa
kwam… Read More
#YALIYOJIRI>>>Dk Phillip Mpango Akataa Kuwa Waziri OmbaOmba,Asema Serikali Haipo Tayari Kukubali Ndoa Za Mashoga Kisa Misaada Ya Wahisani.Fahamu zaidi hapa.
WAZIRI
wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango amesema hatua ya Serikali ya
kukusanya kodi kwa nguvu kwa baadhi ya wafanyabiashara waliotorosha
makontena bila kulipiwa ushuru, haikuwa lengo la kumkomoa mtu, bali
ilileng… Read More
#YALIYOJIRI>>>>Vyama 9 Havitashiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar.Fahamu zaidi hapa.
Maalim Seif Sharif Hamad
Vyama tisa vya siasa kati ya 14 vilivyoshiriki Uchaguzi Mkuu Zanzibar
mwaka jana vimeungana na CUF kutoshiriki uchaguzi wa marudio uliopangwa
kufanyika Machi 20, hadi utakapopatikana mwafaka w… Read More
0 comments:
Post a Comment