Saturday 3 September 2016

#YALIYOJIRI>>>Bulaya: Nimemsamehe Wassira.Fahamu zaidi hapa.

MSUGUANO uliodumu kwa muda mrefu kati ya Esther Amosi Bulaya na Stephen Wassira, umefika kikomo, anaandika Pendo Omary.

Kauli ya Bulaya ambaye ni Mbunge wa Bunda Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) inaakisi kufungua ukurasa mpya dhidi ya hasimu wake wa kisiasa wa muda mrefu na mwanasiasa mkongwe Stephen Wassira.

“Nimemsamehe Mzee Wassiri,” ni kauli aliyoitoa Bulaya wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii leo kuhusu harakati za kisasa jimboni kwake pia hatma ya msuguano kati yake na Wassira uliokuwepo kwa muda mrefu.

Msuguano kati ya Wassira na Bulaya ulianza wakati Bulaya akiwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na muda mfupi baada ya (Bulaya) kuonesha dalili ya kulitaka jimbo hilo lililokuwa likiongozwa na Wassira.

Hata baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, msuguano huo uliendelea na hata Wassira kwenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi kutokana na Bulaya kutangazwa mshundi.

“Sikutegemea kama Wassira angenishitaki, nilitarajia angenipa ushirkiano na kunipa uzoefu ili tufanye kazi nzuri ya kuwapatia maendeleo wananchi wa Bunda Mjini,” amesema Bulaya ambapo maelezo zaidi yamo kwenye gazeti la MwanaHALISI la Jumatatu wiki ijayo.

0 comments:

Post a Comment