Straika
wa Arsenal, Olivier Giroud amemjia juu kiungo wa Paris Saint-Germain,
Marco Verratti kwa mchezo mbaya aliouonyesha na kusababisha apewe kadi
nyekudu katika mechi ya Ligi ya Mabingwa, Jumanne wiki hii.
Giroud
aliingia akitokea benchi katika mchezo baina ya timu hizo uliomalizika
kwa sare ya bao 1-1, lakini alitolewa nje kwa kadi ya pili ya njano
baada ya kuvurugana na mpinzani wake huyo kwenye Uwanja wa Parc des
Princes jijini Paris.
Mwamuzi wa mchezo huo, Viktor Kassai aliamua kuwaadhibu kwa kuwa ubabe wao ulionekana kwa dakika kadhaa walipokuwa wakitunishiana misuli lakini Giroud amenukuliwa akisema:
“Nilipata kadi ya njano ya kwanza sikutaka kuvurugana au kucheza hovyo.
“Verratti aliangua mwenyewe chini, sikuelewa kwa nini. Marquinhos alinisukuma kwa nyuma na sikujua sababu au jinsi gani Verratti alianguka nikaonekana mimi ndiyo nimemchezea vibaya.
“Imenisikitisha sana na nilishangazwa sana na tabia iliyotokea uwanjani.”
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger upande wake alinukuliwa akisema kuwa hakujua kwa nini Giroud alipewa kadi ya pili ya njano.
0 comments:
Post a Comment