Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru watumishi wawili wa Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Martin Chacha na Juma Matandiko baada
ya kuwaona hawana kesi ya kujibum. Uamuzi huo umetolewa leo na Hakimu
Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.
Akisoma
uamuzi huo, Hakimu Shahidi amesema kuwa amewaachia huru washtakiwa
baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi saba wa upande wa
mashtaka na kuona upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha pasipo
kuacha shaka kuwa washtakiwa wametenda kosa.
Washtakiwa Matandika na Mecky wanatuhumiwa kwa kuomba rushwa ya Shilingi milioni 25.
Awali
ilidaiwa kuwa Februari 4 mwaka jana, washtakiwa hao wakiwa waaajiriwa
wa TFF walishawishi kuomba rushwa ya kiasi hicho cha pesa kutoka kwa
Salum Kulunge na Constatine Morandi ambao ni maofisa kutoka Chama cha
Mpira wa Miguu Mkoa wa Geita na Klabu ya Mpira wa Miguu Geita.
Ilidaiwa
kuwa watuhumiwa hao waliomba rushwa hiyo kama kishawishi kwa TFF na
Idara ya Uhamiaji Tanzania kutoa uamuzi dhidi ya klabu ya Mpira wa Miguu
Polisi Tabora ili kuisaidia klabu ya Geita kupanda katika ligi kuu ya
Tanzania.
Akitoa
uamuzi huo, Hakimu Shahidi alisema katika ushahidi uliotolewa na
mashahidi wa upande wa mashtaka unaonesha hakuna mtu aliyeenda Takukuru
kulalamika juu ya washtakiwa kuomba rushwa zaidi ya sauti ya CD kusambaa
katika mitandao.
Amesema upande wa mashtaka haukuonesha kama kweli washtakiwa walitoka Geita kuja Dar Saalam.
Kuhusu
sauti zilizotambuliwa za Mecky na Matandiko kupitia CD, Hakimu Shaidi
amesema watu wana sauti za kufanana na hata kuigizana hivyo hauwezi
kujikita kwenye ushauli kuwa ni washtakiwa wenyewe ndio wanaosikika
kwenye hiyo CD.
Amesema, ni wajibu wa upande wa mashtaka kuthibitisha pasipo kuacha mashakama kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo.
Hakimu
Shahidi ameenda mbali na kueleza kuwa kwa mujibu wa ushahidi ulitolewa
mahakamani hapo, imedaiwa kuwa kanuni za TFF zinaeleza wazi kuwa,
mchezaji akibainika kudanganya ndiye anayepaswa kuadhibiwa lakini si
timu kunyang'anywa pointi.
"Hawa
hawakuwa na mamlaka ya kunyang'anya pointi, hivyo wasingeshtakiwa kwa
kuomba rushwa na hata kama walitenda kosa basi wangeshtakiwa na tuhuma
zingine, labda utapeli", amesema.
Kutokana na upungufu wa ushahidi, Hakimu Shaidi aliwaachia huru washtakiwa kwa sababu hawana kesi ya kujibu.
Kesi hiyo ilikuwa inaendeshwa na Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru),Leonard Swai.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment