Baada ya kupokelewa kwa shangwe katika ukumbi wa bunge leo hii, Rais wa
awamu ya nne, Jakaya Kikwete amesema ni zamu yake kwa sasa kumuunga
mkono mkewe Mama Salma Kikwete.
Kikwete aliyekuwa ameambatana na familia yake, ameshuhudia mkewe akila
kiapo cha ubunge katika kikao cha kwanza cha bunge lililoanza leo mjini
Dodoma.
Salma Kikwete ambaye ni mwenyekiti wa WAMA, alionekana kuwa mstari wa
mbele kumuunga mkono mumewe wakati wa utekelezaji wa majukumu yake ya
kulitumikia taifa.
“Leo asubuhi nmeshuhudia kiapo cha mke wangu, mheshimiwa Salma Rashd
Kikwete kuwa mbunge wa kuteuliwa bungeni Dodoma. Ni zamu yangu kumuunga
mkono,”alinukuliwa Kikwete katika akaunti yake ya twiter.
Kikwete aliingia ndani ya bunge hilo huku akishangiliwa na idadi kubwa ya wabunge wa bunge hilo.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment