Ilibaki
kidogo staa wa Barcelona, Neymar asaini kwa matajiri wa Ufaransa, PSG
kwa kitita cha pauni milioni 42, kabla ya kuitosa ofa hiyo na kuamua
kusalia Barcelona kwa mkataba mpya wa miaka mitano.
Mipango
hiyo ilikuwa ikifanywa kimyakimya katika dirisha la usajili
lililofungwa hivi karibuni, vikao vya dili hilo vikimuhusisha Neymar,
baba yake na Rais wa Klabu ya PSG, Nasser Al-Khelaifi.
Kikao
cha kwanza kilifanyika huko Ibiza, Hispania na Neymar akawekewa mezani
ofa ya kitita cha usajili wa pauni 42m, kukodishiwa ndege anapokuwa na
safari za mechi za Brazil pamoja na kuingia kwenye shea ya baadhi ya
hoteli za matajiri hao.
Pamoja
na yote hayo lakini dili hilo lilikufa katika kikao chao cha pili
kilichofanyika Sao Paulo, Brazil na Neymar kuamua kuongeza mkataba wa
miaka mitano wa kusalia Camp Nou.
Wakala wa Neymar, Wagner Ribeiro amenukuliwa akisema: “Al-Khelaifi alitoa mpaka ofa ya kushughulikia masuala yote ya ushuru wa Neymar atakapokuwa Ufaransa na akamuahidi kuwa mchezaji namba moja wa timu kitu ambacho hawezi kukipata akiwa Barcelona.
“Kulingana na ofa aliyopewa yeye ndiye angekuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani lakini ameamua kubaki Barca kwa kuwa ana furaha akiwa hapo. Nilimtaka aende PSG lakini baba yake alimshauri kubaki Barca.”

0 comments:
Post a Comment