Simba
inatarajia kujitupa dimbani tena Jumamosi ya wiki hii kuumana na Azam
FC lakini tayari imegundua ni sekta gani Azam wanaweza kuitumia kuwazidi
ujanja, hivyo tayari imejipanga kuhusiana na hilo.
Simba
imejinadi kuwa itapambana na timu hiyo kusaka ushindi kwa udi na uvumba
lakini imebaini kuwa Azam inaweza ikabebwa kwa kutumia faida ya nyasi za
bandia zilizopo katika Uwanja wa Uhuru, Dar watakaoutumia katika mchezo
huo.
“Mechi itakuwa ngumu, wote tuna pointi 10 na tuna idadi sawa ya mabao ya kufunga na kufungwa. Wao wanahitaji ushindi kama ilivyo kwetu tunavyouhitaji kwa nguvu zote. Tunafahamu pia wao wamezoea nyasi bandia, tofauti na sisi, hivyo hicho kinaweza kuwa kikwazo kwetu.
“Lakini kama benchi la ufundi tunajua tutafanya nini na hakuna kitakachoharibika, tutalizingatia hilo katika mazoezi yetu na mbinu tutakazojifunza katika maandalizi yetu ya mechi hiyo,” alisema Mayanja raia wa Uganda.
SOURCE: CHAMPIONI
0 comments:
Post a Comment