Manchester United wametangaza kikosi chao cha wachezaji 20 kitakachosafiri kwenda kuvaana na Feyenoord kwenye mchezo wa Europa huku Rooney na Henrikh Mkhitaryan wakitajwa kuachwa kwenye msafara huo.
Jesse Lingard, ambaye alitolewa wakati wa mapumziko kwenye mchezo waliopoteza dhidi ya mahasimu wao Manchester City pia jina lake halipo, huku Antonio Valencia pia akikosekana.
Tayari Jose Mourinho amethibitisha kwamba Marcus Rashford ataanza kwenye mchezo dhidi ya Eredivisie, huku wachezaji kama Timothy Fosu-Mensah na Memphis Depay wakitazamiwa kuanza.
Mkhitaryan, ambaye ameripotiwa kukosa furaha katika klabu hiyo yenye maskani yake Old Trafford kutokana na namba anayochezeshwa, hakujumuika kwenye mazoezi na wenzake mapema kabisa wakati wakijiandaa kuelekea Rotterdam, wakati Phil Jones akiwa ni mchezaji mwingine ambaye hakufanya mazoezi.
Kikosi kizima cha United kinachosafiri hiki hapa: De Gea, Romero, Johnstone; Darmian, Bailly, Blind, Fosu-Mensah, Rojo, Smalling; Carrick, Fellaini, Herrera, Mata, Memphis, Pogba, Schneiderlin, Young; Ibrahimovic, Martial, Rashford.
0 comments:
Post a Comment