Home »
Habari Moto
» #YALIYOJIRI>>>Bodi ya Mikopo Kumwaga Fedha kwa Waombaji wote.Fahamu zaidi hapa.
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imesema wale wote walioomba mkopo mwaka huu na kukidhi vigezo watapewa.
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru alisema hayo juzi mjini
hapa wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti kwa watu watano waliorejesha
mkopo wa elimu ya juu kwa mkupuo na kwa hiari.
Badru alisema idadi ya walioomba mkopo mwaka huu ni wanafunzi 88,000
ambao bodi itahakikisha wale wote waliokidhi vigezo, wanapatiwa fedha
kwa ajili ya elimu ya juu.
Mkurugenzi huyo ambaye amehimiza walionufaika na mikopo kulipa madeni
yao, alisema mwaka jana, wanafunzi waliokopeshwa ni 55,000.
Kuhusu waliopewa vyeti ikiwa ni hatua ya kuwatambua, ni pamoja na
mfanyakazi wa VETA Shinyanga, Richard Jafu aliyerejesha kwa mkupuo Sh
14,749,950 na Francis Mwilafi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo
aliyelipa Sh 15,115,200.
Wengine ni Mbunge wa Vwawa, Japhet Hasunga aliyerejesha Sh 255,000;
Profesa Peter Msoffe ambaye ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha Dodoma
(UDOM) aliyerejesha Sh 1,430,749.
Mwingine ni Mbunge wa Biharamulo, Oscar Mukasa ambaye kiasi
alichorejesha hakikutajwa ingawa mkurugenzi mtendaji wa HESLB, alisema
amerejesha kiasi kikubwa kwa mkupuo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wadau hao walisisitiza umuhimu wa
wanufaika wa mikopo kuirejesha kwa hiari ili kuiwezesha bodi hiyo
kukopesha wanafunzi wengine.
Mbunge wa Biharamulo, Mukasa alishauri bodi hiyo kuangalia uwezekano wa
kurekebisha vigezo kwa lengo la kuwawezesha wanafunzi watokao maeneo ya
pembezoni kunufaika na mikopo hiyo ya elimu. Kwa upande wake, Mbunge wa
Vwawa, Hasunga alisisitiza wabunge wanaodaiwa warejeshe mkopo kwa
mkupuo.
Related Posts:
#YALIYOJIRI>>>>Jeshi la Polisi Latoa ONYO Kali Kwa Vyama vya Siasa.....Ladai Halihitaji Msaada wa Chama Chochote Katika Shughuli za Kiulinzi.Fahamu zaidi hapa.
ONYO
limetolewa kwa vyama vya siasa vinavyojaribu kusuguana na Jeshi la
Polisi kukumbuka kuwa hilo ni jeshi, ambalo liko tayari kutumia nguvu na
rasilimali zote, kuhakikisha raia na mali zao ni salama.
Jeshi
hilo p… Read More
#YALIYOJIRI>>>Mtatiro Amtaka Profesa Lipumba Apumzike Uongozi.Asema CUF Inahitaji Mwenyekiti Mwingine , Adai Hana Mpango Wa Kugombea Uenyekiti.Fahamu zaidi hapa.
ALIYEKUWA
Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Julius Mtatiro amesema hana mpango wa
kugombea nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho, licha ya kuwepo kwa msukumo
mkubwa wa kumtaka agombee.
Katika
taarifa yake aliyoitoa ja… Read More
#YALIYOJIRI>>>>Wakurugenzi Wateule Kukaguliwa vyeti vyao....Ikulu Yaagiza Wafike na Nakala Halisi za Vyeti Kabla Ya Kuapa.Fahamu zaidi hapa.
WAKURUGENZI
wa halmashauri za majiji, manispaa, miji na wilaya walioteuliwa
Jumatano ya wiki hii, wametakiwa kuwasilisha nakala halisi za vyeti vyao
vya taaluma, kabla ya kuapa.
Wakurugenzi
hao wa majiji matano, m… Read More
#YALIYOJIRI>>>>Mnyika ajibu kuhusu taarifa za kumkataa Lowassa, Kuhama Chadema.Fahamu zaidi hapa.
Baada ya kuenea kwa uvumi kuwa Naibu Katiba Mkuu wa Chadema, John
Mnyika anataka kuachana na chama hicho, kiongozi huyo ameibuka na
kukanusha akisema: “Hakuna kitu kama hicho na wala sina mpango wa
kuhama.”
Mnyika… Read More
#YALIYOJIRI>>>>>Viongozi Watatu wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) Watiwa mbaroni Mkoani Dodoma.Fahamu zaidi hapa.
JESHI
la Polisi mkoani Dodoma linawashikilia viongozi watatu wa Baraza la
Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha) Taifa, kwa
uchochezi na kuikashifu serikali.
Pia viongozi hao wanadaiwa kuvaa fulana z… Read More
0 comments:
Post a Comment