Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinatarajia kufanya mkutano wake Mkuu maalum
wa Taifa Machi 12 mwaka huu lengo likiwa ni kufanya marekebisho ya
kanuni na katiba ya chama hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dodoma, Naibu Katibu Mkuu wa
CCM (Bara) Rodrick Mpogolo amesema kuwa pamoja na mambo mengine mkutano
huo pia utafanya kazi ya kujadili na kupitisha marekebisho ya katiba ya
CCM ya mwaka 1977 toleo la 2012 pamoja na kanuni za chama hicho na
jumuiya zake.
Amesema pia mkutano huo utapokea taarifa ya ratiba ya uchaguzi Mkuu wa
CCM na jumuiya zake utakaofanyika nchini kote mwaka huu wa 2017.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment