Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat
Gwajima, mapema leo ametinga katika studio za EFM na TVE, kwa ajili ya kumpa
pole Mkurugenzi Mkuu wa kituo hicho, Majay kutokana na matatizo yaliyomkuta ya
kutuhumiwa kujihusisha na madawa ya kulevya.
“Nipo hapa kwa ajili ya kuwatia moyo na kikubwa niwaambie
tu kuwa Mungu yu pamoja nanyi, hivyo msikatishwe tamaa na mtu au jambo lolote
lile kwani hakuna jaribu lisilokuwa na suluhisho lake.
“Kikubwa zaidi nawaomba mjuwe tu kuwa kila baya linapotokea basi amini mbele yake kuna neema ya bwana inakuja, niwapongeze kwa kuwa na umoja na ushirikiano ambao hata mimi mmenionyesha wazi lakini kikubwa nitaendelea kuwaombea ili Mungu awaongezee ili muweze kuajiri watu wengi zaidi,” alisema Gwajima.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment