Wednesday, 22 March 2017

WAKATI WAZIRI NAPE AKIPOKEA RIPOTI,RC MAKONDA ALIKUWA MBAGALA AKIFANYA HAYA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda leo amezindua visima vitatu vya Maji vilivyopo Mbagala Maji matitu shuleni, amesema kuwa uzinduzi wa miradi hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Maji Ulimwenguni ambayo hufanyika kila mwaka tarehe 22 ya mwezi wa tatu.

Amesema kuwa rasilimali hiyo ni adhimu na ni miongoni mwa rasilimali zinazoathirika sana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
“Naomba nitoe rai kwa kila mmoja wetu kwa nafasi na majukumu aliyonayo katika sekta ya maji, kuanzia watendaji wa Mamlaka zinazohusika na utoaji wa huduma mpaka mtumiaji mmoja mmoja ahakikishe analinda na kutunza vyanzo vya maji,”amesema Makonda.
Aidha, kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “Maji na Majitaka; punguza uchafu yatumike kwa uangalifu” Makonda amewaomba wananchi kuacha kufanya shughuli za kibinafamu kwenye vyanzo vya Maji kama kando kando kwa mto Kizinga uliopo Temeke.
Hata hivyo, Makonda ameipongeza Serikali kupitia DAWASA na wadau wa maendeleo wanaosaidia ujenzi wa miradi hiyo, kwani mbali na kuboresha mazingira ya kiafya, itapunguza matumizi ya maji safi kwa shughuli zisizo za lazima.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizindua kisima cha maji Mbagala Maji matitu leo jijini Dar es Salaam. Kuliani Mkuu wa Wilaya Temeke Mh.Felix Lyaniva.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizungumza na na baadhi ya akina Mama wa Mbagala Maji matitu mara baada ya kuzindua visima hivyo,katika maadhimisho ya wiki ya Maji Ulimwenguni leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimtwisha mama ndoo ya maji marabadaa ya uzinduzi huo.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizindua kisima cha maji Mbagala Maji matitu leo jijini Dar es Salaam. Kuliani Mkuu wa Wilaya Temeke Mh.Felix Lyaniva.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiwasili katika uzinduzi wa visima vya maji Mbagala Maji matitu leo jijini Dar es Salaam

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment