Thursday 5 November 2015

#MICHEZO>>>Timu za Taifa za Afrika Mashariki zapanda viwango vya FIFA huku Timu ya Taifa ya Uganda ikiongoza.Fahamu zaidi hapa.

Katika  Afrika Mashariki  Uganda ndio walio mbele miongoni mwa mataifa ya Afrika Mashariki, wakiwa namba 68 baada ya kupanda hatua saba.

Huku Kenya imepanda hatua sita hadi nambari 125, nayo Tanzania ikapanda hatua moja na kutua nambari 135. 

Huku Timu ya Tanzania Taifa Stars walisonga kwenye mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi kwa ushindi wa jumla wa 2-1 dhidi ya Malawi. Malawi wamo nambari 97 kwenye orodha hiyo.

Rwanda wamo nambari 96 baada ya kushuka hatua tatu nao Burundi nambari 107 baada ya kupanda hatua sita.


0 comments:

Post a Comment