Thursday 5 November 2015

#YALIYOJIRI>>>Masanja Mkandamizaji ajitosa kugombea Ubunge Jimbo la Ludewa akipambana na mdogo wa marehemu Deo Filikunjombe.Fafamu zaidi hapa.


Wagombea tisa wakiwemo mdogo wa marehemu Deo Filikunjombe na mchekeshaji Masanja Mkandamizaji wamejitosa kuwania ubunge wa jimbo la Ludewa, mkoani Njombe kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Uchaguzi wa kumpata mbunge wa jimbo hilo ulilazimika kuahirishwa baada ya kutokea kifo cha aliyekuwa mbunge na mgombea wa jimbo hilo kupitia CCM, Deogratius Filikunjombe.

Miongoni mwa waliojitokeza kwenye kinyang’anyiro hicho ndani ya CCM ni mdogo wa marehemu, Philipo Filikunjombe na msanii wa vichekesho na muimbaji wa nyimbo za injili, Emmanuel Mgaya maarufu kwa jina la ‘Masanja Mkandamizaji’.

0 comments:

Post a Comment