Friday, 6 January 2017

Zaidi ya Mitumbwi 50 na nyavu za kuvulia Samaki zateketezwa.Fahamu zaidi hapa.

Mkuu wa wilya ya Morogoro Bi, Regina Chonjo akiambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ameteketeza mitumbwi zaidi ya 50 na nyavu za kuvulia samaki zipatazo 200 zilizokuwa zikitumika kwenye bwawa la Mindu baada ya wavuvi hao kukaidi amri ya kuacha shughuli hizo ambazo zimekuwa zikisababisha uchafuzi wa maji yanayotumiwa na wakazi wa manispaa ya Morogoro.

Katika kutekeleza zoezi hilo hali ya hewa ikabadilika ghafla baada ya diwani wa kata ya Mindu Hamisi Msasa kusimama katikati ya nyavu na mitumbi iliyokuwa ikichomwa ili kuzuia mitumbwi yake isiteketezwe na kulazimika kukamatwa na askari wa jeshi la polisi na hali ikawa hivi.
 
Akizungumza wakati wa zoezi hilo mkuu huyo wa wilaya amesema alitoa muda wa siku 30 kwa wavuvi wote kuondoa mitumbwi na nyavu katika bwawa hilo lakini cha kushangaza wamekaidi amri hiyo hali iliyomlazimu kuchukua hatua ya kuteketeza zana hizo.
 
Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Moruwasa Mhandisi Nicholaus Angumbwike ameshukuru kufanyika kwa zoezi hilo na kuahidi kuweka ulinzi wa kutosha kwenye bwawa hilo ili kuhakikisha uchafuzi huo haujirudii.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

0 comments:

Post a Comment