Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amesema kutokana na Spika wa Bunge kuteua kibaguzi wajumbe wa kamati za kudumu za Bunge, wabunge wa upinzani hawatashiriki uchaguzi wa wenyeviti wa kamati mbili ambazo zinapaswa kuongozwa na upinzani.
Amedai
kuwa katika kamati hizo za Hesabu za Serikali (PAC) na Hesabu za
Mashirika ya Umma (LAAC), wameteuliwa wabunge wa upinzani ambao hawana
uwezo mkubwa katika kutekeleza majukumu hayo na wamekataa kabisa
kumhamisha na kumuweka Freeman Mbowe kuwa mjumbe wa kamati hizo.
Kwa
mujibu wa Tundu Lissu, ili Mbowe aweze kuwa mwenyekiti wa PAC au LAAC
ni lazima awe mjumbe wake, jambo ambalo limekuwa gumu baada ya Spika wa
Bunge, Job Ndugai, kukataa kumpeleka huko.
Tundu Lissu amesema Ndugai amefanya hivyo kwa madai kwamba amepokea amri kutoka mamlaka za juu asihamishe mjumbe wa kamati zozote ambazo zimetangazwa
Amesema endapo hawataafikiana na Spika na kufanya marekebisho ya wajumbe wa kamati kama wanavyotaka, kamwe hawatakuwa tayari kuongoza kamati hizo
Amesema endapo hawataafikiana na Spika na kufanya marekebisho ya wajumbe wa kamati kama wanavyotaka, kamwe hawatakuwa tayari kuongoza kamati hizo
“Hili
Bunge litakuwa la vichekesho, maana unasema kamati za usimamizi wa
fedha za umma zitaongozwa na wapinzani halafu unawachagulia nani aongoze
hizo kamati. Hatushiriki uchaguzi acha waendelee.”
“Kwa
mujibu wa mabunge ya jumuiya za madola, kamati hizo mbili lazima
ziongozwe na wabunge kutoka upinzani, hivyo majukumu ya PAC hayawezi
kuhamishiwa PIC (kamati mpya ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma).”
Mara
baada ya Spika kutangaza majina ya Kamati za Kudumu za Bunge, wabunge
wa upinzani walipinga jinsi uteuzi huo ulivyofanyika kwa maelezo kuwa
wabunge wenye weledi mkubwa walipangiwa kamati zisizojihusisha na
masuala makubwa ya kitaifa.
Akizungumzia suala hilo, Naibu Katibu wa Bunge, John Joel alisema kamati hizo zinaweza kuendelea na kazi bila kuwa na wenyeviti.
“Kiutaratibu
mwenyekiti wa kamati hizo mbili lazima atoke upinzani ila makamu wake
hutokea CCM. Hata wasiposhiriki zitaendelea na kazi chini ya makamu
mwenyekiti. Hakuna kanuni inayoeleza kuwa lazima kamati iwe na
mwenyekiti. Ni kama bungeni asipokuwepo Spika, shughuli zitaendelea
kufanywa na Naibu Spika,” alisema.
0 comments:
Post a Comment