Mwanafunzi
aliyeongoza katika matokeo ya kidato cha sita yaliyotangazwa jana na
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Hassan Gwaay ameonesha moja kati
ya tunda bora lililodhihirisha faida ya kuanzishwa kwa shule za kata na
Serikali ya awamu ya nne iliyoongozwa na Dk. Jakaya Kikwete.
Gwaay
mwenye umri wa miaka 19 ameeleza kuwa alisoma katika shule ya kata ya
Mirerani Benjamin W. Mkapa mkoani Manyara alipopata elimu ya kidato cha
nne na kupata ufaulu mzuri uliomuwezesha kuchaguliwa kujiunga na shule
ya wavulana ya Tabora (Tabora Boys) kuendelea na elimu yake ya kidato
cha tano.
Amesema
kuwa alipokuwa akisoma katika shule hiyo ya kata, wanafunzi waliokuwa
wanasoma katika shule za watu binafsi zenye mazingira bora zaidi ya
walikuwa wakimuonesha dharau lakini alitaka kuwadhihirishia kuwa hata
katika shule hiyo anaweza kufanya vizuri zaidi yao.
“Sikujali
kelele na dharau za watoto waliosoma kwenye shule za kulipia, ambao
mara kwa mara walikuwa wakiibeza shule yetu. Nilopomaliza kidato cha
nne, nilipata daraja la kwanza alama 10 (Division 1 ya point 10). Ndipo
nilipowadhihirishia kuwa hata kwenye shule za kata watu wanafaulu,” Gwaay anakaririwa na gazeti la Jambo Leo.
Mwanafunzi
huyo ambaye amelelewa na bibi yake kwa muda mrefu baada ya mama yake
kufariki huku akiishi mbali na baba yake (anamsapoti), alisema kuwa
baada ya kujiunga na shule ya wavulana ya Tabora kusoma masomo ya
Fizikia, Kemia na Hesabu (PCM), aliweka bidii zaidi hasa baada ya
kugundua kuwa wanafunzi aliokutana nao hapo wote walikuwa na akili sana.
Alisema
kuwa alipofanya mtihani wa ‘Mock’ alipata Fizikia (A), Kemia (A) na
Hesabu (B) na kwaba aliumia sana kuona amepata B. Aliongeza bidi hadi
kuibuka na alama A kwenye mitihani yote katika Mtihani wa Taifa na
kutangazwa kuwa mwanafunzi aliyeongoza.
Changamoto
ya upungufu wa walimu hususan wa Sayansi katika shule nyingi za umma
nchini lilimkumba pia Gwaay katika shule ya wavulana ya Tabora, lakini
aliipanda ngazi hiyo ndefu kwa nguvu ya ziada bila kukata tamaa.
“Hakuwa
na Mwalimu wa Fizikia pale. Tangu najiunga sikuwahi kumwona zaidi ya
wakuazimwa ambaye alikuwa akija jioni na mwisho mwa wiki tu na alikuwa
akija mara chache. Muda mwingi tulitumia kujisome wenyewe lakini
hatukukata tamaa,” alisema.
Shule
ya wavulana ya Tabora mwaka huu imerudi kwenye nafasi yake ya ubora
ulioaminika miaka mingi iliyopita. Imeshika nafasi ya 5 kati ya shule
zote.
0 comments:
Post a Comment