Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira amewasimamisha kazi watumishi watatu wa Jeshi la Polisi kwa
tuhuma za kufanya malipo hewa, yaani kulipa posho ya chakula (Ration
Allowance) kwa watu ambao sio askari
Hatua
hii ni mwendelezo wa uchunguzi wa tuhuma za kufanya malipo hewa ya
kiasi cha sh. 305,820,000/= zilizopelekea kusimamishwa kazi kwa Mhasibu
Mkuu wa Jeshi la Polisi Bw.Frank Charles Msaki wiki iliyopita.
Kwa
Mamlaka ya Katibu Mkuu chini ya Kanuni ya 35(2)(b) ya Kanuni za
Utumishi wa Umma za mwaka 2003 zikisomwa pamoja na Kanuni ya 37 ya
Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003, Kuanzia tarehe 13 Julai, 2016,
amewasimamisha kazi wafuatao: Bw. Damian Aloys Bupamba ambaye ni
Mhasibu Daraja la II na Bi, Ida Dennis Moyo Mhasibu Daraja la I kwa
makosa ya kufanya malipo ya posho ya chakula kwa watu wasiostahili kwa
kipindi cha kuanzia mwaka wa fedha 2013/2014 hadi 2015/2016.
Aidha
kwa Mamlaka ya Katibu Mkuu chini ya Kifungu cha 7(4) cha Sheria Na.8 ya
Tume ya Utumishi wa Jeshi la Polisi na Magereza ya Mwaka 1990 kama
ilivyorekebishwa na Sheria Na. 8 ya mwaka 2015 kikisomwa pamoja na
Kanuni C.23(1)(b) ya Kanuni za Utumishi wa Jeshi la Polisi za mwaka 1995
zilizorekebishwa mwaka 2013, kuanzia tarehe 13 Julai, 2016,
amemsimamisha kazi Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Milambo Mwita
Milambo kwa makosa ya kufanya malipo ya posho ya chakula kwa watu
wasiostahili kwa kipindi cha kuanzia mwaka wa fedha 2013/2014 hadi
2015/2016.
Watumishi
wote watatu wamehusika kufanya malipo haya jambo ambalo ni kinyume na
Kanuni F.9 ya Kanuni za Utumishi wa Jeshi la Polisi za mwaka 1995 kama
zilizovyorekebishwa mwaka 2013.
Katibu
Mkuu amewasimamisha wahusika hawa ili kupisha Uchunguzi wa tuhuma dhidi
yao unaofanyika kufuatia Uchunguzi Maalamu wa Mkaguzi wa Ndani wa Jeshi
la Polisi uliobaini makosa ya malipo hewa.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
0 comments:
Post a Comment