Wednesday, 31 August 2016

#Breaking News>>>Mbowe Atangaza Kuahirisha Maandamano ya Oparesheni UKUTA Yaliyokuwa Yamepangwa Kufanyika Kesho.Fahamu zaidi hapa.

Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo ametangaza kusitishwa kwa maandamano ya Oparesheni UKUTA yaliyokuwa yamepangwa kufanyika kesho nchi nzima.

Mbowe ametoa kauli hiyo ya kuahirisha maandamano mchana huu wakati akiongea na vyombo mbalimbali vya habari.

Amesema sababu kubwa za kuahirisha maandamano hayo ni busara za viongozi wa dini ambao wameiomba Chadema iwape muda wa   kutafuta Suluhu 

Mbowe amesema maandamano hayo yameahirishwa hadi Oktoba Mosi

Msikilize hapo chini akiongea

#Breaking News>>>LIVE STREAM KUTOKA MAKAO MAKUU YA CHADEMA KUANZIA mchana huu.

MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI NA KAMATI KUU YA CHADEMA 31/08/2016

#BURUDANI>>>>FAIZA Ally 'Napenda Kuvaa Nusu Utupu, Najipenda Nilivyo Bomba Najua Wengi Mnatamani'.Fahamu zaidi hapa.

Mrembo Faiza Ally Ameamua Kufunguka haya Hapa Chini:

"Napenda kuvaa half naked - Na najipenda kujiangalia nilivyo bomba Na kuangalia watu wanavyo niponda.... najue wengi mnatamani lkn Ndio hivyo tumeumbwa tofaut....
Msinifananishe na mtu mwenye mzigo nyuma#hakunaga star mnene duniani hlf pia msinifananishe na wenye vijuso Kama katuni - mi niko Na class beauty 😉 I AM DIFFERENT" Faiza Ally

#YALIYOJIRI>>>>Makusanyo Kodi za Simu Yapanda Maradufu.Fahamu zaidi hapa.

Sheria ya Fedha ya Mwaka 2016 iliyopitishwa kuhusu utozaji ushuru kwenye ada ya kutuma na kupokea fedha kwenye miamala ya benki na simu, imeanza kuzaa matunda kutokana na ongezeko la mapato lililoanza kushuhudiwa kutoka kampuni za simu.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu iliyokutana jana na Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), iliambiwa kutokana na sheria hiyo iliyopitishwa Bunge baada ya kupitisha bajeti ya mwaka huu, mwezi uliopita serikali imeshuhudia ongezeko kubwa la mapato, yaliyotolewa na kampuni za simu.

Taarifa hiyo ilitolewa jana kwenye Kamati ya Kudumu ya Miundombinu, imeonesha Kampuni ya Vodacom ilikuwa ikitoa kodi ya ushuru wa bidhaa kwa fedha zinazotumwa kwa wastani wa Sh milioni 360 kwa mwezi, lakini baada ya mabadiliko ya sheria, Julai pekee mwaka huu imelipa Sh bilioni 1.9.

Mwakilishi wa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Godwin Barongo aliiambia kamati hiyo kuwa kwa upande wa Kampuni ya Tigo, walikuwa wanatoa wastani wa Sh milioni 250 kwa mwezi, lakini sasa wametoa Sh bilioni 1.48.

Barongo ambaye ni Meneja Msaidizi, Kitengo cha Walipa Kodi Wakubwa TRA alikuwa akizungumzia namna Mtambo Maalumu wa Kusimamia Mawasiliano na Udhibiti wa Mapato yatokanayo na Simu (TTMS) unaosimamiwa na Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) ulivyowezesha kufanikisha ukusanyaji mapato.

“Pamoja na mabadiliko ya sheria yaliyoanza mwezi Julai mwaka huu, kampuni za simu zilikuwa zikitoza transfer, lakini sheria ilikuwa haigusi kwenye kutoa, Baada ya hiyo, tuligundua kuwa sasa kamisheni nyingi zilipelekwa kwenye kutoa kwa sababu hakuna tozo na kwenye transfer zinapungua,” alisema Barongo.

Aliendelea kusema, “Kwa hiyo mabadiliko haya ya sheria ya sasa hivi ambayo tunatoza kwenye kuweka na kutoa, yametusaidia.” 

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso alisisitiza kuwa wabunge wanategemea Wizara ya Miundombinu kupitia sekta ya mawasiliano, ichangie mapato mengi kwa serikali.

Baada ya Bunge kupitisha mabadiliko ya sheria ya fedha yaliyopitisha utozaji kodi ya ushuru wa bidhaa katika miamala ya benki na simu za mkononi, ulijitokeza mjadala ambao baadhi ya watu walidai ushuru huo utaathiri wateja wa kampuni za simu na benki.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alifafanua kwamba serikali imeamua kutoza ushuru kwenye ada ya kutuma na kupokea fedha au vyote kwa kadri itakavyotozwa akisisitiza kwamba utalipwa na benki na kampuni na si mtumiaji au mpokeaji wa fedha katika miamala itakayofanyika.

#BURUDANI>>>DIAMOND ANUNUA GARI JIPYA LENYE THAMANI YA ZAIDI YA BILIONI MOJA YA KITANZANIA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Huenda Diamond Platnumz akawa ameitimiza ndoto aliyokuwa nayo kwa miaka mingi – kumiliki gari alipendalo zaidi, Rolls Royce.
Kwa muda mrefu, staa huyo amekuwa akisema kuwa hilo ndilo gari analotaka kulimiki kiasi cha kujipa jina ‘The Rolls Royce Musician From East Africa.’

Diamond ambaye yupo jijini Los Angeles, Marekani alikoenda kushoot video ya wimbo aliomshirikisha Ne-Yo, ameshare kipande cha video kwenye Instagram cha gari hilo na kuashiria kuwa huenda akawa amelinunua tayari.

Weka Picha za Utupu Mtandaoni Uende Miaka 20 jela – TCRA.Fahamu zaidi hapa.

Unataka kwenda jela? Ni rahisi, weka picha za ngono mtandaoni, na utakuwa mkazi wa huko kwa kipindi cha miaka 20.
Kwa mara nyingine tena, mamlaka ya mawasiliano Tanzania, TCRA imewakumbusha watanzania kutozichezea sharubu za sheria ya makosa ya mtandaoni, lasivyo wataishia pabaya.

“Ni vyema wananchi wakatambua kwamba uchochezi kwenye mitandao kwa kusambaza ujumbe wenye viashiria vya uvunjifu wa amani au kuweka picha zisizofaa kwenye mitandao sheria ipo wazi na watu watajikuta wanaishia pabaya, hivyo ni vyema kuchukua tahadhari mapema,” alisema Mhandisi wa Mawasiliano wa Victoria Rulakara wakati akizungumza kwenye kipindi cha Hotmix cha EATV.

Wakati huo huo, mamlaka hiyo imeendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi sahihi ya mitandao ikiwa ni pamoja na kuwaonya watu wanaonzisha blog zenye majina ya uongo kutukana watu wengine.

Sheria ya Makosa ya Mtandaoni ilipitishwa mwaka jana na rais mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete.

#BURUDANI>>>>Afande Sele Mikononi Mwa Polisi Morogoro.Fahamu zaidi hapa.

Msanii mkongwe wa muziki kutoka Morogoro, Afande Sele amedai anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Morogoro kwa madai anagawa pesa kwa watu ili kuwashawishi wajitokeze katika maandamano ya UKUTA ambayo yamepigwa marufuku.
Afande

Rapper huyo ambaye ni mwanasiasa na aligombea ubunge kupitia cha ACT Wazalendo katika uchaguzi uliyopita, amedai yupo mikononi mwa polisi toka jana.

“Huku ni kushindwa kama sio kufeli, toka jana nipo mikononi mwa polisi eti naambiwa nimeratibu mkutano wa UKUTA , nimechapisha T-shirt na kugawa fedha ili kesho watu waandamane, pia kuaandaa mkutano maeneo ya Msamvu.,” aliandika Afande Sele kupitia facebook yake.

Aliongeza, “Nina zaidi ya mwezi sijakaa maeeneo ya Msamvu zaidi ya kupita nikiwa naelekea mikoani tena nikiwa kwenye gari yangu. Ila hii aibu na fedheha kwa jeshi la polisi, maamuzi ya kukurupuka . Tusubiri,”

#MICHEZO>>>>ASAMOAH GYAN AKWAMA KUJIUNGA NA KLABU YA ENGLAND.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Uhamisho wa mkopo wa muda mrefu (msimu mmoja) wa hodha wa Ghana Asamoah Gyan kuhamia klabu ya Reading inayoshiriki ligi daraja la kwanza (Championship) umekwama.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu ya Sunderland alitarajiwa kujiunga na The Royals akitokea klabu ya Shanghai SIPG ya nchini China.

Kwa mujibu wa BBC, Gyan, 30, hatajiunga tena na klabu hiyo baada ya ripoti kutoka kwamba amefeli vipimo vya afya

Gyan alifunga magoli 10 kwenye Premier League wakati akiitumikia klabu ya Sunderland kabla ya kwenda kucheza soka kwenye falme za Kiarabu.

#BURUDANI>>>Wema Sepetu: Sirudi Tena Dar.Fahamu zaidi hapa.

Malkia wa filamu Wema Sepetu amelikimbia jiji la Dar es salaam na kuamua kuanzisha makazi mapya mkoani Arusha kama alivyodai mwenyewe.
Mwigizaji huyo ambaye kwa sasa yupo mkoani Arusha ameonyeshwa kuvutiwa na jiji la Arusha na kuamua kuwarusha roho mashabiki wake kwa kuwaambia kwamba hatarudi tena Dar es salaam.

“My shouger nikimpenda hovyooo, kweli watu tumetoka mbali, huyu ndiye atakayenifanya nihamie Arusha kwakweli,” aliandika Wema katika picha hiyo hapo juu akiwa na rafiki yake.

Kadhi siku zinavyozidi kwenda mrembo huyo anaonyesha kuendelea kuvutiwa mji wa Arusha.

“Nirudie nini Dar mie, kurudi Dar majaliwa, na sirudi Dar ng’o,” aliandika Wema katika ujumbe wake wa pili.

Hata hivyo uwamuzi huyo umepokewa tofauti na baadhi ya mashabiki wake katika mitandao ya kijamii.

Haya ni maoni ya baadhi ya mashabiki wake.
Hopeolivier24
Dar bila Wema Itawezekana kweli? Itakuwa manispaa maana jiji unaliamishia Arusha😀😀

Zai_miss
Kwaiyo ushahamia arusha jamani khaaaa vigoma vyako itakuwaje My mmmh ila umefanya lamaana maana bongo kwa moto arusha Baridi kishezi😂😂😂😂😂

Theonerealdully
Utarudi tuu. Watu wa dar miji mingine hamuiwezi hekaheka zenu na mafoleni mwayapenda hivyohivyo

Andymsalali
jamn kwann, rudi bhana, tumekuzoea wenyew kukuona dar

Zeyaabdallah
Wema Rudi home coz matatizo hayakimbiwi dadaangu mpenz Wang.sawa Bali unatakiwa uyakabi

Bongo5

#YALIYOJIRI>>>>Lowassa Atoa Waraka Kuhusu Kukamatwa Kwake.Fahamu zaidi hapa.

WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ametoa waraka akisema kitendo cha askari wa Jeshi la Polisi kuwakamata wakati wakiwa kwenye kikao cha ndani cha Chadema jana  kimemuimarisha na kumpa nguvu zaidi ya kudai demokrasia.

Katika waraka wake kwa vyombo vya habari leo, Lowassa amesema anafurahishwa na kutiwa moyo na jinsi Watanzania walivyoipokea operesheni yao ya Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta) iliyopangwa kuanza kesho kwa maandamano na mikutano, lakini vitendo vya polisi vinawapa wasiwasi wananchi.

Lowassa, akiwa na Freeman Mbowe, ambaye ni mwenyekiti wa Chadema, John Mnyika (naibu katibu mkuu-Bara) na viongozi wengine wa chama hicho kikuu cha upinzani walikamatwa jana wakiwa kwenye kikao cha ndani kilichofanyika Hoteli ya Girrafe na baadaye kwenda kituo kikuu cha polisi kwa mahojiano kabla ya kuachiwa na kutakiwa kwenda kituo hapo kesho.

#BURUDANI>>>WEMA Sepetu Acharuka..Amshukia Vikali Aliedai Amepata Bwana Mpya Arusha.Fahamu zaidi hapa.

Mrembo Wema Sepetu amemfungukia mtu anae eneza maneno kwenye mitandao kuwa amepata bwana mpya mkoani Arusha ambapo yupo hivi sasa
Maneno hayo yamemkuna Wema Sepetu na kuamua Kumshukia mtu aliyesema hayo maneno, Soma hapa chini:



‘Soooooooo, Rumor has it That huyu mkaka ndo New Baby…. Maskini ya Mungu…! First & Foremost, Nimeongea nae kwa simu akaniomba niweze kuwa MC and special appearance at his birthday party… I got my paycheck and did my work… Sasa sielewi Mipuuzi na Mi***** inayotokwa mapovu kuuutwaaaaa kunifatilia na maisha yangu…. Nd mimi nasemaje lets jus assume it was True, Ni maisha yangu ryt…. So i dont know where all These Bia**** with LowLives wanakuja na kuanza kufatilia wats goin on in my Life…. God…!!! Nimewakosea nini Mungu wangu…. Maisha yangu yamekuwa ni deal kwenu…. Naongea na wewe unaeuza Nchi za waarabu…. Leave me and my Life alone… I keep saying this jamani, Sijawahi bother na maisha ya mtu… I do my shit…. Huyu kaka simjui na nimemjua on da nyt of his Birthday…. Hata kumuwish sijamuwish…. Nimewish mtu mwingine Birthday ila mijitu mifala inatokwa mapovu….. Sasa labda niseme hivi, Wema ana maisha yake nd anaishi atakavyo yeye… Maisha ya Wema hayamuhusu mtu yoyote mwingine….. And again, My heart belongs to someone else…. Nd I love my baby tooo much…. So mkiwa mnaandika vitu vyenu vya kipuuzi…. Again Im talking to you, Stupid Bi-polar Biatch…. Uwe una uhakika….. Kwani unachotaka kwangu ni nini Mbwa wewe… Wallahy never have I done this in my Life, But this has just pushed my buttons to da extent that I cannot take it anymore…. Nimekaa kimya muda mrefu sana and I aint a person dat talks too much… Ila napigiwa simu nyingi mpaka za demu wake na huyu Ally akilalamika and I had to do this…. I keep telling you unatia huruma, You need a Hug… But nat from me honey… Waarabu siku hizi hawalipi nini…? Usiharibie watu bwaana… Afu ni sababu nilikukataa kuwa karibu na mimi ndo maana umenikaa rohoni au…. Maana nakuskia tu unaongeeaaa utasema u r my Mom…. Leave me the Fuck alone…!!! una bahati sana nina wisdom ila leo ningekutukana mbwa wewe… But naaaaaah I got my siblings tena wadogo goin thru my page so I wouldnt want them to see things they shudnt…. But wewe Nyau… Kuna kitu unachokitafuta kwangu and utakipata soon…. If it wasnt for my baby nisingefanya huu upuuzi But My baby comes first…. I had to do this’. -Wema Sepetu

#YALIYOJIRI>>>>Lowassa, Mbowe Watakiwa Kuripoti Polisi Keshoi Septemba 1.Fahamu zaidi hapa.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho, Edward Lowassa na viongozi wengine waandamizi wameitwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwenda kuripoti kesho Septemba Mosi.


Hatua hiyo inatokana na viongozi hao kukamatwa juzi, baada ya kufanya mkutano maalumu wa ndani wa Kamati Kuu, na walipelekwa Kituo Kikuu cha Polisi cha Kanda hiyo na kuhojiwa kabla ya kuachiwa.



Mbali na Mbowe na Lowassa, viongozi wengine wa Chadema waliokamatwa na kutakiwa kwenda Polisi kesho ni Katibu Mkuu, Vincent Mashinji, Naibu wake, John Mnyika na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, Said Issa Mohammed.



“Wameitwa Polisi waende Septemba mosi kuripoti baada ya jana kukamatwa na kuhojiwa wakituhumiwa kukiuka maagizo ya Polisi,” alisema Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene na kufafanua:



“Lakini wanaweza kwenda au wakaanzia kwenye maandamano kisha wakaenda Polisi kuripoti.”



Alisema maandamano hayo yatakuwapo kama yalivyopangwa kwani maandalizi yake yamekamilika.



Habari zaidi zilieleza, kwamba jana mchana viongozi hao walikuwa wakifanya kikao Makao Makuu ya chama hicho Kinondoni Dar es Salaam, ambapo pia walikutana na wabunge wote wa chama hicho kwa makundi tofauti.



Kwa mujibu wa mtoa habari ndani ya Chadema makao makuu katika kikao hicho walijadili mambo mengi ikiwa ni pamoja na suala la utekelezaji wa Ukuta kesho.



Mmoja wa wabunge wa Chadema alisemai kwamba walikuwa wakiwekana sawa kuhusu maandamano yao.



Alibainisha kwamba katika mkutano huo ambao Mbowe hakuwepo pia walijadili maombi ya viongozi wa dini kuwataka kusitisha maandamano hayo Septemba mosi.



“Viongozi wa dini wamekuwa wakituomba tusitishe maandamano ya Ukuta Septemba mosi, tusubiri hadi baada ya mkutano wa vyama vya siasa Septemba tatu,” alisema Mbunge huyo wa Kanda ya Ziwa.



Aliongeza: Katika mkutano huo, Lowassa na viongozi wengine walijadili hayo na ikikubalika kwa heshima ya viongozi wa dini maandamano ya Ukuta yafanyike baada ya Septemba tatu.”



Hata hivyo, mwandishi alishuhudia wabunge wengi wa chama hicho wakitoka katika mkutano huo kimya kimya bila kutaka kuzungumza na kabla muda uliopangwa kwisha, huku taarifa zikieleza kwamba mkutano huo uliahirishwa baada ya kuwepo taarifa za kutaka kuvamiwa na Polisi.



“Tumeambiwa tusambaratike, tutajulishwa wapi tutakutana tena, kama hapa au wapi,” alidokeza mmoja wa wabunge hao.



Baada ya mkutano huo kuahirishwa, Lowassa alitoka eneo hilo huku taarifa zikieleza alikuwa akielekea kwenye moja ya hoteli jijini humo kuungana na Mbowe ambapo walikuwa na mazungumzo na baadhi ya viongozi wa dini.

#YALIYOJIRI>>>>Ndege za Kivita Kutawala Anga la Dar Septemba 1.Fahamu zaidi hapa.

Septemba mosi mwaka huu inataraji kuingia katika histori ya Tanzania kutokana na matukio ambayo yanataraji kufanyika siku hiyo, matukio hayo ni pamoja na sherehe za miaka 52 ya Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ), maandamano ambayo yamepangwa kufanywa ya UKUTA na tukio la kupatwa kwa jua.

Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati alipokutana na Maafisa wa Jeshi la JWTZ Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alisema JWTZ inapotimiza miaka 52 ni fahari kubwa hivyo tunapaswa kuwapongeza kwa kudumisha amani na mshikamano.

Alisema Jeshi hilo limejipanga kurusha angani ndege zake za kivita katika anga la Dar es Salaam, Septemba 1 mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya kuanzishwa kwake.

Makonda aliwataka wananchi kutokuwa na hofu wanaposikia ngurumo za ndege hizo bali wafurahie kwani ni ndege zao.

“Mnaposikia milio ya ndege zetu mbalimbali, mfurahie kwa sababu hizo ni ndege za wananchi. Usisikie muungurumo ukashtuka. Hakuna jambo lolote lile zaidi ya kuonesha vifaa vyetu na jinsi ambavyo wanajeshi wetu kwa miaka 52 wamaeendelea kuwa imara na vifaa vizuri,” alisema Makonda.

Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa waliwataka wananchi waliojipanga katika vikundi mbalimbali kuripoti kwa wakuu wao wa wilaya kujiandikisha ili waweze kushiriki pamoja na Jeshi hilo katika zoezi la usafi jijini humo.

Aliwataka wakazi wa mkoa huo pia kujitokeza kuchangia damu katika vituo mbalimbali ambavyo vimeanishwa ili kuunga mkono juhudi za uchangiaji damu zitakazofanywa na wanajeshi wa JWTZ.

“Hii ni sehemu ya amani, tufanye usafi kwa amani. Tujitolee damu zetu kwa amani na mwisho wa siku tuwaenzi na kuwapongeza wanajeshi wetu kwa kazi kubwa wanayoifanya,” Makonda alieleza.

Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Mkoa aliendelea kutoa onyo kwa watu watakaotaka kufanya maandamano yaliyopigwa marufuku ya oparesheni UKUTA akiwataka kutii sheria.

“Mimi ninavyojua UKUTA ni kuwa mtu amefika mwisho wa kufikiri sasa kama watakuwa wamefika mwisho wa kufikiria basi sisi tutawasaidia … watu wapo wanapanga kufanya mambo ya kusaidia jamii wao wanapanga maandamano nawashauri wananchi waungane na Polisi,” alisema Makonda.

Tuesday, 30 August 2016

#MICHEZO>>>HUYU MCHEZAJI WA MPIRA AVUNJIWA MKATABA WAKE BAADA YA KUGUNDULIKA ANA HIV.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Zikiwa zimepita siku nne tu tangu asajiliwe na klabu ya Al Ittihad inayoshiki ligi kuu ya Misri, Samuel Nlend, 21, mkataba wake umevunjwa baada ya klabu yake mpya kugundua mchezaji huyo anamaambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU).

Jarid linalojulikana kwa jina la KingFut.com limeripoti kuwa, afisa habari wa klabu hiyo amethibitisha taarifa hiyo ya kusikitisha kwa vyombo vya habari.

Mshambuliaji huyo ameitumikia Cameroon katika michezo mitano, alifunga goli January kwenye michuano ya mataifa ya Afrika kabla ya kujiunga na Al Ittihad majira ya kiangazi.
Samuel Nlend alisaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia Al Ittihad tangu tarehe 24 August. Licha ya hayo yote kutokea bado amepata support ya kutosha kutoka kwa klabu yake mpya ya Misri.

#YALIYOJIRI>>>Tamko La Mtandao Wa Watetezi Wa Haki Za Binadamu Dhidi Ya Mauaji Ya Askari Wa Jeshi La Polisi.Fahamu zaidi hapa.

Mtandao wa Watetezi wa Waki za Binadamu (THRDC) kwa niaba ya wanachama wake tunalani vikali maujai ya askari wa jeshi la polisi huku tukisisitiza kwamba askari wa jeshi la polisi wanaofanya kazi katika misingi na sheria ni watetezi wa haki za binadamu kama walivyo watetezi wengine. 

Kutokana na taarifa rasmi ya jeshi la polisi ni kwamba mnamo tarehe 23/08/2016 saa moja usiku maeneo ya Mbagala Mbande kata ya Mbande Temeke, majambazi ambao idadi yao haikuweza kufahamika wakiwa na silaha za moto walivamia benki ya CRDB tawi la Mbande ambapo waliwashambulia na kuwaua askari wanne wa Jeshi la Polisi waliokuwa kazini na kuwajeruhi raia wawili waliokuwa jirani na eneo hilo. 
 
Askari waliofariki katika tukio hilo ni E,5761 CPL Yahaya, F,4660 CPL Hatibu, G9524 PC Tito na G.9996 PC Gastone na raia waliojeruhiwa ni Ally Chiponda na Azizi Yahaya wote wakazi wa Mbande. 
Katika tukio hilo, majambazi hayo yalifanikiwa kupora silaha mbili za SMG na risasi sitini (60) na hakuna pesa au mali za benki iliyoibiwa, ni dhahiri kwamba walikuwa na kusudio la kujipatia silaha kwa ajili ya kufanya uhalifu na si vinginevyo kama baadhi walivyotaka kupotosha. 
Ikumbukwe kuwa majambazi mara kadhaa mwaka jana katika maeneo mbalimbali chini, mfano Kituo cha Stakishari Dar es Salaam na Kituo cha Polisi Ikwiriri , vilivyamiwa na majambazi kwa lengo la kuchukua silaha kwa ajili ya uhalifu.
 
Aidha, Tunalipongoza Jeshi la Polisi kwa kuweza kuwafikia majambazi hao huko Mkuranga bila kuumiza raia. Pia tunatoa pole kwa familia za askari wote watano waliopoteza maisha wakiwa kazini. 
Askari anaekamilsha idadi ya askari waliouwawa kufika watano ni Askari Thomas Njiku,Mkuu wa Kitengo cha Kuzuia Ujambazi alieuwa Vikindu wilayani Mkuranga wakati akiongoza kikosi maalum cha kuwasaka watu waliosadikiwa kuwa ni majambazi waliotekeleza tukio la kihalifu la Mbade,Mbagala.
 
Tunawasihi Watanzania kutoipokea dhana inayotaka kujengwa na wanasiasa kuwa hatukemei matukio haya dhidi ya polisi. 
Kumbukeni kuwa Mtandao wa Watetezi umekuwa ukitoa matamko mbali mbali kukemea mauaji ya askari wa jeshi la polisi, na tumekuwa mara kwa mara tukisisitiza kwamba askari wa jeshi la polisi ni watetezi wa haki za binadamu, kwa kuwa jukumu lao la kwanza ni kulinda mali za watu na usalama wa binadamu. 
Mtandao unatambua kuwa askari wa jeshi la polisi pia ni ndugu zetu, kaka zetu na baba zetu hivyo madhila wanayokumbana nayo ni yetu sote.
 
Mfano, katika repoti ya hali ya watetezi wa haki za binadamu kwa mwaka jana(2015) , Mtandao uliweza kuwa na kipengele maalumu kilichozungumzia haki za polisi na hali ya usalama kwa polisi wakiwa kama watetezi wa haki za binadamu.
 Katika ukarasa wa 18 wa repoti hiyo Mtandao uliweza kurekodi matukio ya uvamizi na mauaji ya jeshi la polisi zaidi ya kumi (10) na wengine watano (5) wakiachwa wamejeruhiwa. Kwa maana hii tukio lilitokea Mbagala ni muendelezo wa matukio ya kiuhalifu yanayoendelea nchini. 
 
Kumekuwa na changamoto kutoka kwa Jamii kuwatambua askari wa jeshi la polisi kama watetezi wa haki za binadamu, na hii ni kutokana na ukweli kwamba baadhi ya askari wamekuwa wakitumia vibaya madaraka yao kukandamiza haki za wananchi. 
Hali ilivyo sasa inaweza kuharibu dhana nzima ya polisi kuwa ni walinzi wa raia na mali zao, kwani vitendo wanavyofanya polisi dhidi ya raia hasa wafuasi wa vyama vya siasa na viongozi wao ni sababu kubwa ya kuharibu uhusiano mzuri kati ya polisi na raia.
 
Mtandao unatambua kwamba jeshi la polisi ni mamlaka muhimu sana katika kustawisha amani na ulinzi wa nchi kama litakuwa huru, bila kuingiliwa na wanasiasa na kuegemea upande wowote. 
Mtandao unapenda kuona kwamba Jeshi la Polisi linafanya kazi kwa weledi na kwa mujibu wa sharia na katiba ya nchi. Aidha, Mtandao unaona pamoja na migongano mbali mbali ya kazi za polisi na za wanasiasa ( hasa nafasi za wakuu wa mikoa na wilaya), ni vyema polisi wakaangalia misingi ya kimataifa ya haki za binadamu ili kuhakikisha usawa mbele ya jamii ili kurudisha mahusiano mazuri baina ya polisi na jamii wanayoitumikia.
 
Sambamba na hayo, Mtandao pia umesikikitishwa na kauli ya Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Mhe Paul Makonda aliyotoa tarehe 25 agosti 2016 wakati wa kuaga miili ya askari wanne waliouwawa huko Mbande Mkoani Dar es Salaam. Mtandao unakemea matamshi ya aina hiyo kutoka kwa kiongozi yoyote Yule, kwakuwa matamshi kama haya yanakwenda kinyume na misingi ya utawala bora na haki za binadamu na yanaweza kuwa sehemu ya kupoteza amani ya Taifa. Kitendo cha kukejeli haki za binadamu na kuamuru askari polisi wapige tu bila kujali taratibu za kisheria kinakwenda kinyume na misingi ya utawala bora.
 
Tunapenda viongozi wa serikali watambue kwamba kazi ya kulinda na kutetea haki za binadamu ni ya kikatiba na ndiyo maana kupitia Katiba yetu tuna Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora iliyoundwa kwa lengo la kuhakikisha viongozi wanaheshimu misingi ya utawala bora na haki za binadamu. Watetezi wa haki za binadamu wanatambulika kote duniani na wanalindwa kisheria mfano, kimataifa tuna Tamko la watetezi wa haki za binadamu la mwaka 1998. 
 
Madhara ya Uhusiano Mbaya kati ya Polisi na Raia
Ili Jeshi la Polisi liweze kufanya kazi yake vizuri ya kupambana na uhalifu hawana budi kuhakikisha wanakuwa karibu na wananchi. Madhara ya kutokuwa na mahusiano mazuri kati ya Jeshi la Polisi na raia ni makubwa. 
 
• Mojawapo ya madhara ni pamoja na kukua kwa makosa ya jinai na polisi kukosa taarifa za waalifu toka maoneo mbalimbali.
• Hali ya makosa ya jinai Tanzania imezidi kukua katika kiwango kikubwa. Kukua kwa makosa ya jinai ni zao la kutokuwa na mahisiano mazuri kati ya raia na polisi.
Wito wetu;
• Mtandao unatoa pole kwa Jeshi la Polisi pamoja na familia za askari hao na tunatoa wito kwa askari wengine wa jeshi la polisi kuendelea na kazi zao kwa weledi huku wakiboresha mahusiano mazuri na wananchi.
• Tunaishauri serikali kuliongezea nguvu Jeshi la polisi na kuboresh utalaamu katika kufanya kazi zao
• Tunawasihi askari wa Jeshi la wananchi kuheshimu mipaka ya kazi zao na kuheshimu haki za binadamu na katiba ya nchi katika kutekeleza kazi zao za kila siku
• Tunaishauri serkali kuwe na mabadiliko katika mfumo wa jeshi la polisi kuanzia kwenye mfumo wa kisheria ambao utatoa wajibu na uwajibikaji na kuheshimu haki za binadamu
• Tunaomba umma kutoa taarifa kwa jeshi la polisi na vyombo vya usalama hasa pale wanapohisi kuna tukio linalo ashiria uvunjaji wa amani na usalama.
• Tunaiomba serikali yetu kuipa kipaumbele jeshi la polisi katika kuboresha vitendea kazi vyao,nyumba za kuishi na mishahara bora ili kukidhi hali ya maisha ya sasa.
• Tunawaomba wadau wengine wa Haki za Binadamu pamoja na mashirika mengine ya maendeleo kukemea vikali tukio hilo. Tunashauri viongozi wa siasa waache kuingilia kazi za polisi ili kuepuka migogoro
 
PICHANI  JUU :Wakili wa THRDC akiwaonyesha waandishi wa habari(hawapo pichani) repoti ambayo ilitolewa na THRDC juu ya hali ya Watetezi wa Haki za Binadamu kwa mwaka jana(2015) ,ambayo ina kipengele maalumu kilichozungumzia haki za polisi na hali ya usalama kwa polisi wakiwa kama watetezi wa haki za binadamu katika ukarasa wa 18 wa repoti hiyo, http://thrdc.or.tz/download/situation-report-2015/
 
Imetolewa na Onesmo Olengurumwa
Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC)
 
Imewasilishwa na Bennedict Ishabakaki
Wakili wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC)
 
30/08/2016

#BURUDANI>>>King Crazy GK Aamua Kuacha Muziki wa Rap..Sasa Kuimba Kama Diamond.Fahamu zaidi hapa.

Rapa kutoka kundi la East Coast, King Crazy GK ameamua kuingia Studio kwa Alonem ambapo amebadili maudhui ya uimbaji wake kutoka kurap na kufanya muziki wa kuimba huku video akiifanya na muongozaji Donald kutoka Uganda.
Akipiga story ndani ya eNewz, GK amesema kuwa ushindani uliopo kwenye game la muziki tofauti na zamani ikiwa ushindani ulikuwa wa hapa tu nchini, Ila kwa sasa wameongezeka wasanii mbalimbali wanaotoka hata nje ya nchi ya Tanzania.

“Nimeamua kuimba lakini ni kutokana na game la Tanzania kubadilika, zamani tulikuwa tukishindana sisi wa Tanzania kama Juma Nature, AY na wengine lakini kwa sasa muziki wa Bongo ume'change' na kuingia mpaka wakina Wizkind, so kubadilika muhimu” amesema GK.

Hata hivyo GK amebadilisha kabisa aina ya muziki wake na kutengeneza ngoma yenye mahadhi tofauti kabisa na muziki wake huku mwenyewe akisema anaandaa mashambulizi makali ili kupambana na game la sasa.

Taarifa Kwa Umma Kuaribika Kwa Mashine ya MRI Hospitali ya Taifa Muhimbili.Fahamu zaidi hapa.

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) inapenda kuujulisha umma kwamba mashine ya MRI itasimama kwa muda kufanya kazi baada ya kuharibiika. Mashine hii iliharibiika tarehe 24/08/2016 baada ya kutokea hitilafu ya umeme.

Baada ya kuharibiika, tarehe hiyo (24/08/2016) mafundi wa Philips kwa kushirikiana na mafundi wetu walianza kutafuta athari baada ya kutokea kwa hitilafu ya umeme.

Tarehe 26/08/2016, mafundi walibadilisha betri zote 31 na kufunga mpya ili kuongeza ufanisi katika mashine hii kwa kuwa betri za awali zilikuwa zimefungwa muda mrefu. Tarehe 28/08/2016 mafundi walibaini kwamba kifaa cha Gradient Module kilikuwa kimeharibiika na tayari hospitali kwa kushirikiana na Philips wameagiza kifaa hicho kutoka Uholanzi.

Hospitali ya Taifa Muhimbili inawaomba radhi wananchi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.

Imetolewa na;

                                                                                         John Stephen, Ofisa Uhusiano,
                                                                                        
                                                                                         Hospitali ya Taifa Muhimbili

HII NDO Hoteli mpya Tanzania, wateja hulipa shilingi milioni 22 kwa usiku mmoja.Fahamu zaidi hapa.

Hoteli hii iko katika kisiwa cha Thanda kusini mwa Tanzania. Ina vyumba 5 vya kulala ambapo itakugharimu shilingi milioni 22 kulala hapo kwa usiku mmoja.

Hoteli hii inaakadiriwa kuwa na ukubwa wa ekari 20 ikiwa imezungukwa na viumbe mbalimbali wakuvutia waliomo ndani ya maji. Hoteli hii inapakana na kisiwa cha Mafia, unaweza kufika kwa kutumia helikopta kutokea Dar es Salaam, au kwenda kwa ndege hadi Mafia na kisha kutumia boati maalum kwa ajili ya wateja.

Ukiwa katika hoteli hii unaweza kufurahia mambo mbalimbali kama kuogelea, uvuvi, diving. Hoteli hii inamilikiwa na Christin na Dan Olofsson kutoka nchini Sweden. Walikuwa na ndoto za kutafuta eneo ambalo halijakaliwa na watu na kutengeneza sehemu tulivu ya kupumzika, na ndipo wakalipata eneo hilo Tanzania.

#YALIYOJIRI>>>>UVCCM Waahirisha Maandamano Yao,watii Agizo La Jeshi La Polisi.Fahamu zaidi hapa.

Agosti 22, 2016 Umoja wa Vijana wa CCM tuliutangazia umma na dunia kwamba ifikapo Agosti 31 mwaka huu tutaitisha maandamano ya amani nchi nzima yenye lengo la kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk John Pombe Magufuli kwa utendaji wenye tija, ufanisi na uliorudisha imani na matumaini kwa wananchi.

Msimamo na dhamira ya kufanya maandamano hayo ya amani yenye maudhui na kusudio hilo, bado uko pale pale ingawaje si kwa tarehe tuliopanga na kutangaza awali yaani Agosti 31 mwaka huu.

Jumuiya yetu kama mjuavyo ni ya Vijana wa CCM, (UVCCM) inapata malezi kwa karibu mno na Jumuiya ya Wazazi ya CCM. Wiki ya jana Mwenyekiti wa Wazazi Taifa Nd. Abdallah Bulembo alikutana na waandishi wa habari akitutaka UVCCM tuahirishe maandamano ya Agosti 31 mwaka huu hadi wakati mwingine.

Kwa mujibu wa Katiba ya Chama Cha Mapinduzi, Jumuiya ya Wazazi ndiyo Msimamizi wa Malezi, Maadili na Adabu kwa Vijana wote nchini, sisi UVCCM tunaamini kuwa sikio halishindani na kichwa, mtoto ni mtoto kwa Wazazi wake hakui, hana jeuri wala ubishi.

Mtoto au watoto wanaokaidi amri, ushauri au maelekezo ya Wazazi wao huitwa watukutu, wenye viburi, manunda na wasioambilika. UVCCM si watukutu, hatukufunzwa tuwe wabishi, wakaidi na wenye viburi. Tumezingatia kutii maelekezo, makatazo na maonyo , tumeambiwa tuahirishe maandamano yetu nasi tumekubali na kuheshimu mambo tuliyoaswa.

Sambamba na hilo tumepata majibu ya barua yetu tuliyomwandikia Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP Ernes Mangu) inayotutaka tuache kufanya maandamano yetu kwa sababu Polisi wamezuia mikutano ya hadhara ya Vyama vya Siasa na maandamano nchi nzima.

Jambo jingine ambalo limetufanya pia tuahirishe maandamano yetu ya Amani ni taarifa ya kintelejinsia iliowasilishwa na Kamati yetu ya Usalama na Maadili ya UVCCM mbele ya kikao cha Sekreteriet yetu, nayo ilipendekeza  suala hilo liahirishwe kwa wakati huu hadi muda mwingine.

Pia jambo jingine ambalo limefanya maandamano hayo tuyabatilishe ni kulipisha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ ) ambalo litakuwa katika shughuli za maadhimisho miaka 52 tokea kuanzishwa kwake.

Wanajeshi wetu watakuwa katika kazi mbalimbali za kijeshi kwenye kambi zao na mitaani kufanya usafi wa mazingira, hivyo isingependeza na wala si heshima wakati sisi tukiandamana, wao wakifanya kazi muhimu kila mmoja wetu zinazomgusa badala yake ni vyema kuwaunga mkono jambo wanalolifanya la usafi wa mazingira.

UVCCM tumekubali, hatutaki kuingia katika uvunjaji wa sheria hasa baaada ya kutakiwa kuahirisha na mamlaka za Kisheria hadi wakati mwingine muafaka na si wakati huu.

Tunaelewa kwamba uamuzi wetu wa awali wa kutaka kuandamana kwa amani hata kama tungenyimwa kibali ungetugharimu, ungetusababishia madhara na pengine hasara, kwa wakati huu na kuona jambo lenyewe ni la kuipa Ari serikali katika kuhimiza Uwajibikaji, Utendaji na Usimamizi bora wa Uendeshaji wa masuala ya kiutawala.

Tulishusha maagizo kwa Makatibu wetu wote wa Mikoa yote 32 na Wilaya 171 ya Kichama tukiwataka waandike barua katika Ofisi za Ma RPC na OCD, washirikiane ili kuratibu maandamano na kuyafanikisha kama tulivyokusudia.

Watendaji wetu wa ngazi husika wamefuata maelekezo, wametii taratibu zetu za kiutendaji na leo tumewajulisha tena wasitishe maandamano hadi tutakapowapa tena maelekezo mengine. Tunawahimiza na kuwataka ni vyema kutii mamlaka za Kikanuni na Kisheria.

UVCCM kwa wakati huu tumeamua kuachana na maandamano badala yake tunajikita katika matayarisho ya kuwapeleka Vijana wetu wakashiriki katika Mafunzo ya Siasa, Utawala, Uongozi, Ufundi na Ujasiriamali yatakayoanza kufanyika katika Chuo chetu kilichopo huko Ihemi Mkoani Iringa ambapo kitakuwa kielelezo na alama nzuri ya kumuunga mkono Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kwa vitendo.

Tumewataka Makatibu wetu wa Mikoa na Wilaya kuendelea na zoezi la Uratibu na Uhakiki kwa Vijana ambao watateuliwa kushiriki Mafunzo hayo huko Ihemi.

UVCCM tunarejea kusema tena kwamba dhamira ya maandamano yetu ya kusifu Utendaji wa Serikali ya awamu ya tano iko pale pale ila tutapanga tarehe nyingine katika wakati ujao badala ya kufanyika Agosti 31 mwaka huu kama tulivyotangaza hapo awali.

UVCCM tunawataka Vijana wote kuendelea kuheshimu Tunu ya Amani Umoja na Mshikamo wetu kwa Taifa.


KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Shaka Hamdu Shaka (MNEC)
KAIMU KATIBU MKUU.

#YALIYOJIRI>>>>HAKIKA KWA HII SHOW ALIYO FANYA DIAMOND NCHINI KENYA ..HAWEZI SAHAULIKA KAMWE ..AMEACHA HISTORIA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Diamond Platnumz ana miaka mingi ya kuvuna mapesa kutokana na show zake. Kutoka kwenye mapokezi yaliyovunja rekodi, Meru nchini Kenya hadi kuangusha show iliyohudhuriwa na makumi kwa maelfu ya mashabiki wenye kiu, staa huyo ameendelea kujiweka kwenye ligi yake mwenyewe. Jionee

#YALIYOJIRI>>>Serikali Kutoa Ajira Mpya 71,496 Hivi Karibuni.Fahamu zaidi hapa.

SERIKALI imeanza kuwashughulikia watumishi walionufaika na fedha za watumishi hewa ambapo hadi sasa watumishi 839 wapo katika hatua mbalimbali wakiwemo waliofikishwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na wengine wanaendelea kuhojiwa polisi kwa ajili ya kufikishwa mahakamani.

Sambamba na hilo, serikali inatarajia kutoa ajira mpya 71,496 kwa mwaka huu wa fedha baada ya kukamilisha uondoaji wa wafanyakazi hewa. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Angella Kairuki aliyasema hayo wakati akizungumzia utekelezaji wa mipango na mikakati ya wizara yake katika kipindi cha ‘Tunatekeleza’ kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1). Kairuki alisema,

“Kwa sasa tayari wapo watumishi wameshahojiwa na kuchukuliwa maelezo yao polisi na upelelezi utakapokamilika watachukuliwa hatua mbalimbali za kisheria, ikiwemo kufikishwa mahakamani… Tunakamilisha ushahidi na tutawatangazia tutakapokamilisha,” alisema.

Alisema waligundua kwamba kuna maofisa utumishi na wahasibu ambao siyo waaminifu, badala yake walikuwa wakielekeza fedha kwa ndugu zao na miradi yao na wengine walishastaafu lakini bado majina yao yalikuwa yakiendelea kupokea mishahara wakati walitakiwa kuondolewa kwenye mfumo.

Alisema kwa kipindi cha Machi mosi hadi Agosti 20 mwaka huu, watumishi hewa waliogundulika ni zaidi ya 16,127 na kuisababishia serikali hasara ya mabilioni ya fedha. Kwa kipindi cha Agosti pekee watumishi hao hewa wangelipwa mishahara wangeisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh bilioni 16.

“Uhakiki huu ni endelevu na tumegundua changamoto kubwa katika usimamizi wa mishahara ni uadilifu kwa watu waliokasimiwa madaraka. Maofisa Utumishi, Maofisa Utawala na Wahasibu wamepewa madaraka lakini wengi wao siyo waaminifu, hivyo kwa sasa tumeweka uwajibikaji kwa waajiri,” alisema.

Aidha alisema wanaufanyia mfumo wao maboresho zaidi ili uweze kuchakata taarifa nyingi zaidi ambapo pia sekta ya mishahara imeshushwa katika ngazi za chini zaidi hasa katika sekta za elimu na afya ambazo zimekutwa na watumishi hewa wengi zaidi ili waweze kuwa na taarifa za mtumishi mmoja mmoja.

Alisema upo muongozo ambao fedha za serikali zinaporejeshwa zinapitia hazina na kusisitiza kwamba wataendelea kuhakikisha wanasimamia fedha zote ambazo zilichukuliwa serikalini kinyume na utaratibu na isivyo halali zinarudishwa kwa mfumo sahihi.

Pia alisema wameongeza kasi ili kuhakikisha kunakuwa na nidhamu ya kazi na uwajibikaji kwa watumishi wa umma, hivyo wanaanda mkataba wa utendaji kazi kwa watumishi wa umma na ikiwezekana utaanza kutumika mwaka ujao wa fedha.

Alisema serikali imefanya maboresho makubwa katika mishahara na motisha kwa ajili ya maslahi ya watumishi wa umma, sambamba na kuhimiza taasisi mbalimbali kuweka vitendea kazi ili kuwawezesha wafanyakazi kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Akizungumzia ajira hizo mpya Kairuki aliwatoa hofu watanzania waliokuwa wanatarajia ajira serikalini na kusisitiza kwamba walichokuwa wanasubiri ni takwimu halisi kwa taasisi ili kujua ni watumishi wangapi wameondolewa.

“Baada ya kukamilisha mchakato huo, hatua nyingine zitaendelea… Hii ni neema kwa waliomaliza vyuo, cha msingi wavute subira maana tutatoa ajira 71,496 kwa mwaka huu wa fedha na hatukuzifuta ajira. 

"Nawashauri vijana wasijiingize kwenye makundi yasiyofaa wasubiri ajira zinakuja,” alisema. 

Katika hatua nyingine, Kairuki alisema, wamepokea malalamiko zaidi ya 200 kutokana na ukiukwaji wa sheria ya maadili ya viongozi wa Utumishi wa Umma ambayo inamnyima mtumishi kutotumia madaraka yake vibaya.

“Katika malalamiko hayo 142 yanahusu sheria ya maadili. Sekretarieti ya Maadili imefanya uchunguzi wa awali na malalamiko 12 yataanza kufikishwa Baraza la Maadili na hatua mbalimbali zinaweza kuchukuliwa ikiwemo kushushwa vyeo au kuachishwa kazi,” alisema.

Pia aliwaagiza maofisa utumishi kuwahudumia watumishi na kuwapa haki zao ikiwemo kuwapandisha madaraja kwa wakati pale wanapostahili. Aidha Kairuki alikemea tabia ya baadhi ya watu kughushi taarifa za utumishi wa umma na kusisitiza kwamba jambo hilo ni kosa kubwa kwa yeyote anayefanya hivyo.

“Mtu yeyote ambaye anatoa nyaraka za serikali na siyo mlengwa au anayetoa nyaraka ambayo imewekewa zuio kwa mujibu wa sheria ni kosa la jinai na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake. Tunawasisitiza watumishi wa umma kuhakikisha wanazingatia sheria hizo na mwongozo wa utoaji nyaraka na kumbukumbu za taarifa za serikali,” alisema.