Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Elimu, Joseph Mungai unatarajiwa kuagwa   Dar es Salaam leo katika viwanja vya Karimjee.
Akizungumza
 na waandishi wa habari jana, mtoto wa marehemu, William Mungai alisema 
ibada ya kuuaga mwili huo itafanyika katika viwanja hivyo saa 5.00 
asubuhi.
Hata
 hivyo mtoto huyo wa marehemu hakutaka kuingia kwa undani kuhusu chanzo 
cha kifo cha baba yake, badala yake alisema familia iachwe iendelee 
kushauriana na daktari.
Alisema
 pamoja na hayo, kifo hicho kimewashtua kwa vile  kimetokea ghafla na 
kwamba baada ya kuisha kwa ibada ya kuaga mwili huo, utasafirishwa hadi 
Mafinga, Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa kwa mazishi.
“Hadi
 sasa familia tunajua kwamba marehemu aliugua tumbo la kawaida na 
tulimpeleka hospitalini ambako alifariki dunia, tunaomba familia iachwe,
 kwa sababu  bado tunashauriana na daktari wake.
“Tumekubaliana mwili wake uagwe kesho (leo) saa tano Viwanja vya Karimjee ambako pia historia yake yote na familia itasomwa,” alisema William.
Kifo
 cha Mungai kilitokea juzi jioni katika kile kilichoelezwa kuwa   
alianza kujisikia vibaya baada ya kunywa kiywaji katika   hoteli moja 
iliyopo Msasani, ambayo aliizoea.
Mmoja
 wa waombelezaji waliofika nyumbani kwa marehemu jana ni pamoja na Naibu
 Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)- Zanzibar, 
Salum Mwalimu ambaye alimwelezea Mungai kuwa aliunga mkono  mabadiliko 
ya siasa.
“Hakuwa
 na kadi ya Chadema lakini alipenda mabadiliko, mwanaye William 
aligombea ubunge wa Mafinga kupitia  Chadema na baba yake alimuunga 
mkono,” alisema.
Mbunge
 wa zamani wa Kwela, Chrisant Mzindakaya alisema amesikitishwa na kifo 
hicho ikizingatiwa wiki iliyopita walikuwa pamoja na walizungumza mambo 
mengi ya siasa.
“Hakuwa
 na kesho katika maisha yake, alilokuwa na uwezo wa kulifanya alilifanya
 siku hiyo hiyo, alikuwa na msimamo, hakukubali kuyumbishwa,” alisema Mzindakaya.
Wakati
 huohuo, mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta unatarajiwa 
kuwasili leo ukitokea  Ujerumani ambako alikuwa akitibiwa hadi mauti 
yalipomfika.
Taarifa
 zilizotolewa na msemaji wa familia ya marehemu, Gerald Mongella, 
zinasema  mwili huo utawasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa 
Julius Nyerere saa 9.00 mchana na kupelekwa nyumbani kwake Msasani, Dar 
es Salaam.
“Ijumaa(kesho)
 saa tatu asubuhi ibada ya kuuaga mwili huo itafanyika katika viwanja 
vya Karimjee ambako ndugu na wakazi wa   Dar es Salaam watapata fursa ya
 kuaga,” alisema Mongella.
Mwili
 wa Sitta utasafirishwa hadi Dodoma ambako utaagwa na wabunge na baadaye
 utasafirishwa kwenda Urambo kwa mazishi   Jumamosi.
Sitta
 alifariki Novemba 07 mwaka huu katika Hospitali ya Technal University 
alipokuwa akipatiwa matibabu ya maradhi ya saratani ya tezi dume.
 









 




 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment