Home »
Michezo
 » #MICHEZO>>>HECTOR BELLERIN AMDENGULIA GUARDIOLA AJIFUNGA KITANZI KWA WENGER.FAHAMU ZAIDI HAPA.
 
Maisha ni safari ndefu ambayo ina 
mabonde na milima, wakati matokeo ya uchaguzi mkuu wa Marekani 
kutangazwa sasa turejee katika michezo na burudani na hapa tunapiga hodi
 pale kwa washika bunduki wa London Arsenal ambao tayari wamekata utepe 
mara baada ya kuongeza mkataba kwa beki wake ambaye alikuwa anagombaniwa
 na vilabu vikubwa vya Barcelona na Manchester City.
Hector Bellerin ameonesha kiwango cha 
hali ya juu tangu ajiunge na timu hiyo akitokea timu ya watoto ya 
Barcelona na amekaa kidogo timu B ya Arsenal ndipo akapata namba ya 
kudumu na kufanya maajabu, kiwango alichokionesha kikubwa sana.
Hii imemfanya apate shavu dodo 
kwa ‘Gunners’ kutokea mshahara wa pauni elfu 10,000 hadi kupewa pauni 
lakini moja 100,000 kwa wiki ni mshahara mkubwa sana, mkataba huo 
utagharimu kiasi cha pauni milioni 30 ,mkataba  utaisha hadi 2022. 
Hii inatufundisha tusikate tamaa kwani 
hii inaweza ikakufanya wewe uzidi kujituma na ujue lazima upate unacho 
kihitaji . Wakati tunasubiri mchezo wa wiki ijao pale Old Trafford kati 
ya Arsenal na Manchester United.
 
 
0 comments:
Post a Comment