Unaweza
kusema hii ni hali ya kushangaza, wachezaji watatu wa Taifa Stars,
wameachwa nchini kutokana na kutokuwa na hati za kusafiria ‘passport’
kwa ajili ya safari yao kwenda nchini Zimbabwe.
Kikosi
cha Stars kimeondoka jana mchana kuelekea Zambabwe kwa ajili ya mchezo
wa kirafiki wa kimataifa utakaochezwa kesho Jumapili kwenye Mji wa
Harare nchini humo.
Wachezaji
walioachwa ni James Josephat kutoka Prisons, Said Kipao (JKT Ruvu) na
Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting, huku Omar Mponda wa Ndanda
akibadilishiwa ndege kutokana na passport yake kuchelewa, hivyo
alitarajiwa kuondoka jana jioni.
Pale
kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar,
lilishuhudia kikosi hicho kikiondoka huku changamoto nyingine ikiwa ni
baadhi ya wachezaji nyota kusahau passport majumbani mwao.
Kuhusiana
na hilo Mkwasa alisema kuwa licha ya kutofanya maandalizi ya kutosha,
lakini anaamini watarudi na matokeo ya ushindi huku akithibitisha
kuachwa kwa wachezaji hao.
“Tunakwenda
kupambana kwa sababu malengo yetu ni kurudi na ushindi ambao utasaidia
kutupandia katika viwango vya Fifa ingawa maandalizi yetu yamekuwa ni
madogo sana,” alisema Mkwasa.
Kwa
upande wake nahodha wa Taifa Stars anayekipiga Klabu ya KRC Genk ya
Ubelgiji, Mbwana Samatta alisema: “Maandalizi kifupi yapo vizuri kwa
sababu kila mchezaji ametoka kwenye ligi tuna imani tutashinda."
SOURCE: CHAMPIONI
Bonyeza Hapa CLICK HERE
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
Bonyeza Hapa CLICK HERE
0 comments:
Post a Comment