Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison
Mwakyembe amesema watumiaji wa mitandao ya kijamii Tanzania ni wengi
sana hivyo mitandao hiyo kama haitadhibitiwa mapema huenda ikaleta
matatizo katika nchi.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe.
"Watanzania ambao wapo kwenye mitandao ni mamilioni kwa sasa, lakini
tunachosema tatizo hapa ni matumizi mabaya ya hiyo mitandao, mwanasiasa
maarufu wa Marekani nafikiri Clinton alisema mwaka jana kuwa matumizi
mabaya ya mitandao ni ugonjwa hatari unaoweza kuteketeza dunia, kwa
kweli mitandao ya jamii kama hatujaiangalia vizuri au kuithibiti inaweza
kutuingiza katika matatizo makubwa sana" alisisitiza Mhe. Dkt Harrison
Mwakyembe
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment