Bajeti ya Wizara ya Afya imewasilishwa bungeni leo na Waziri Ummy Mwalimu akisema kuwa malaria imeendelea kuwa changamoto nchini, licha ya kugawa vyandarua na kupulizia dawa katika mikoa mbalimbali.
Amegusia mambo mbalimbali ikiwemo kuwataka wenye dalili za kifua kikuu wajitokeze kwa kuwa kinatibika.
"Wenye ukimwi kuanzia Juni wanapewa dawa za kupunguza makali bila kujali kupungua kwa CD4."
"Watoto 2020 wamefanyiwa upasuji wa vichwa vikubwa na mgongo wazi Muhimbili" Amesema Mwalimu
Pia
amesema hudumu za kusafisha damu na figo zimeanza kupatikana katika
hospitali za kanda. Amezilaani halmashauri zote ambazo hazikutoa fedha
za mfuko wa maendeleo ya wamawake
Kuhusu mauaji ya wazee, Waziri Ummy amesema yamepungua kutoka 190 mwaka 2015 hadi 134 mwaka 2016.
Waziri
Ummy ametaja vipaumbele vya wizara yake ambavyo ni kuimarisha kinga
na tiba, huduma za mama na watoto, upatijanaji wa dawa, kuimarisha vituo
vya afya na hospitali, kuimarisha huduma lishe, matumizi ya tehama na
kuongeza wanaotumia bima ya afya.
Ameeleza
hakuna mjamzito atakayefariki kwa kukosa dawa ya kuzuia kifafa cha
mimba na amesema zimetengwa Sh 7 bilioni kwa ajili yake.Amesema
wajawazito 150,000 watapewa bima ya afya ili waweze kujifungua salama
Waziri
Ummy amesema yeye si Daktari lakini ameshakuwa 'bush doctor' na ameomba
Sh1,115,608,772,090.Fedha kwa ajili ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na
Watoto ni Sh37,906,880,090.Jumla ya fedha za fungu la Afya ni
Sh1,077,701,892,000
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza HapaFollow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment