Friday, 5 May 2017

Hali ya Mbunge wa CHADEMA Siyo Nzuri, Alazwa Muhimbili.

Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche alifikishwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jana akitokea Dodoma kwa ajili ya matibabu baada ya kyzidiwa ghafla.

Mbunge huyo anasumbuliwa na uvimbe ambapo mdogo wake, Edward Heche amesema kuwa kaka yake alianza kupatwa na maumivu makali juzi (Jumatano) akiwa Dodoma ndipo alipokwenda kwa ajili ya kumsaidia.

“Nilifika Dodoma saa tisa nikamkuta anatibiwa katika Hospitali ya Bunge hali yake haikuwa nzuri alikuwa analalamika kuwa maumivu yalizidi, tukampelekea Hospitali ya Mkoa bado aliendelea kulalama huko akapewa dawa za kupunguza maumivu lakini haikusaidia tulipoandikiwa kuja Muhimbili,” amesema na kuongeza;

“Hali ya Heche sio nzuri, tatizo ni kwamba alifanyiwa upasuaji kwenye uvimbe uliokuwa pajani lakini kwa bahati mbaya inaonekana baadhi ya nyuzi ziliachia na ndiyo inamsababishia maumivu makali.



Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa 

0 comments:

Post a Comment