Friday, 5 May 2017

Mauaji mengine yatokea Rufiji.

Rufiji.Mtu mmoja Aitwae Amri Chanjale (55), mkazi wa kitongji cha Makaravati katika Kijiji cha Umwe Kusini wilayani Rufiji ameuawa kwa kupigwa risasi akiwa nyumbani kwake.

Tukio hilo limetokea jana saa 1.30 usiku baada ya watu wasiojulikana kufika kwake na kutekeleza shambulio hilo.

Marehemu huyo ambaye pia ni mwanachama wa CCM ameuawa ikiwa ni baada ya siku tano kuuawa kwa  Mohammed Malinda ambaye nae alikuwa ni mwanachama wa chama hicho.

Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM wilayani Rufiji, Musa Nyeresa amethibitisha kuuawa kwa mwanachama huyo kwa kupigwa risasi.



Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa 

0 comments:

Post a Comment