Mbunge wa Kigoma mjini kupitia tiketi ya ACT, Zitto Kabwe ameukosoa
mpango wa serikali kuanza kujenga reli ya kati baina ya Dar es Salaam na
Morogoro na kusema serikali inapaswa kuangalia vipaumbele vya maeneo
ambayo shughuli za reli hiyo itasaidia
Zitto amebainisha hayo wakati akichangia hotuba ya Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano katika mkutano wa Bunge Jijini Dodoma kwa
kumtaka Waziri Profesa Makame Mbarawa aangalie takwimu ni wapi anapaswa
apeleke reli ili aweze kupata pesa ya kujenga reli nyingine.
"Toka mwaka jana tumelalamika kuhusu jambo hili...Nawashukuru wabunge
wemametoa tafsiri mpya ya reli ya kati, reli ya kati tafsiri yake ni
Kigoma Dar es salaam au Dar es salaam Kigoma maeneo mengine yote ni
matawi ya reli ya kati......
"Lakini ujenzi wa 'Standard Gauge' kwa hatua hizo wanazoziita za awali
unatoka Dar es salaam kwenda Mwanza....Namuomba Waziri aangalie takwimu
ni wapi atapeleka reli ili apate pesa ya kujenga reli nyingine.......
"Takwimu zinaonesha kwamba mizigo ambayo Tanzania inahudumia kwa nchi za
maziwa makuu ni tani Milioni tano kwa mwaka kwa mujibu taarifa ya hali
ya uchumi mwaka 2015/2016.
"Katika hizo asilimia 34 ni Zambia, asilimia 34 ni Kongo, asilimia 12 Rwanda, aslimia 6 Burundi, asilimia 2.6 Uganda...
"Unapoanza na 'Standard Gauge' matailion ya fedha ukaipeleka Isaka na
Mwanza maana yake ni kwamba unaenda kuhudumia mizigo aslimia 15 ya
mizigo yote tunayoipitisha unaacha kwenda kuhudumia mizigo asilimia 40
kwa maana ya Kongo na Burundi ambayo yote inapita Kigoma". Alisema Zitto
Aidha, Zitto amehoji wizara pamoja na serikali kuwa ni njia gani
walizozitama mpaka kuamua kupeleka sehemu ambayo wanajua haiwezi kuleta
faida kwa taifa.
"Economics' gani ambazo mmetumia katika kuhakikisha kwamba reli inaelekea mahali ambako hakuna mzigo..
"Sipendi kusema kwamba Kigoma inatengwa siyo lugha ambayo mimi kiongozi
napenda kuzungumza lakini hili takwimu zote zinaonesha reli inapaswa
kwenda kule ambako kuna faida, hampeleki kule ambako kuna faida ambako
kuna faida hii maana yake nini ?...
"Lakini siyo hivyo tu Waziri, kuna fedha za Benki ya Dunia ...kwaajili
ya ukarabati wa reli hata hizi Bilioni 200 za ukarabati wa reli ambao
upo sahizi na zenyewe mmepeleka kule kule mnapopeleka 'Standard Gauge',
mnashindwa hata kutudanganya kwa pipi". Alihoji Zitto
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment