Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amesema wamekamilisha safari ya kuwapeleka Marekani majeruhi watatu wa ajali iliyoua wanafunzi 32, walimu wawili na dereva wa Shule ya Lucky Vincent ya Arusha.
Akizungumza leo (Alhamisi) katika ofisi ya mganga mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, Nyalandu amesema ndege maalumu ya kuwabeba majeruhi hao imetolewa na Shirika la Samaritan Fund la nchini Marekani ambayo itawasili kesho.
Nyalandu amesema rubani anatarajiwa kuwasili jijini Arusha leo akitokea Nairobi nchini Kenya na iwapo kila kitu kitakamilika safari itakuwa Jumamosi.
"Watakaoondoka ni abiria wanane, ambao ni majeruhi na wazazi wao, muuguzi mmoja na daktari mmoja. Hati za kusafiria ziko tayari, kinachosubiriwa ni viza," amesema Nyalandu.Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment