Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), imeingia mkataba wa miaka mitatu kuidhamini Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars wenye gharama ya shilingi bilioni 2.1 za Kitanzania.
Katika
pesa hizo, Serengeti watakuwa wakiipa Taifa Stars shilingi milioni 700
kila mwaka, huku pesa zingine zikiongezeka kutokana na makubaliano
waliyoafikiana wakati wa kutiliana saini mbele ya Waziri wa Habari,
Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe.
Akizungumza
wakati wa kusaini mkataba huo, mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo,
Helen Weesie, amesema: “Tunaona fahari kuiunga mkono Taifa Stars na
tumeamua kuchukua fursa hii ya kuidhamini tukifahamu fika mchango
unaotolewa katika sekta ya michezo katika maendeleo ya kiuchumi na
kijamii.”
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Naye
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, aliishukuru
kampuni hiyo kwa uungwaji mkono wake huku akisema kwamba itasaidia
katika maandalizi ya timu hiyo kuelekea mechi za kufuzu fainali za Kombe
la Mataifa Afrika (Afcon) pamoja na ile inayowahusisha wachezaji wa
ndani (Chan).
Ikumbukwe
kuwa, hii ni mara ya pili kwa kampuni hiyo kuidhamini taifa Stars kwani
mara ya kwanza iliingia mkataba wa udhamini kuanzia mwaka 2007 mpaka
2011.
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment